Katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga – siku ya tarehe ya18 Oktoba, klabu ya Simba itacheza mechi ya kujiandaa na klabu kubwa ya South Africa.
Simba ambayo iliondoka nchini jana keshokutwa (Jumamosi)
itacheza mchezo wa kirafiki na Orlando Pirates mjini
Johannesburg, Afrika Kusini.
Katika mchezo huo, Simba SC
itawakosa wachezaji wake walio timu
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na
Uganda, The Cranes- ambao
wanatarajiwa kujiunga na wenzao
kuanzia Jumatatu.
Hata hivyo, mshambuliaji Mganda,
Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga
na The Cranes yeye hatakwenda
kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu
yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi
ya kufuzu AFCON katikati ya wiki.
Wachezaji wa Simba SC walioko Stars
ni; Miraji Adam, Joram, Mgeveke,Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
Simba SC imefikia katika hoteli ya
Eden Vale Petra na itakuwa inafanya
mazoezi kwenye viwanja wa Eden
Vale mjini Johannesburg.
Post a Comment