SIMBA
ipo mkoani Mbeya kujiandaa kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya
Tanzania Prisons, keshokutwa lakini straika wa Simba, Amissi Tambwe
ametoa kauli ambayo inaweza kuwa bado inawaumiza vichwa mashabiki wengi
wa timu hiyo.
Tambwe amelia kutokuwa na bahati msimu huu lakini akasema kuwa yeye
mwenyewe anashangazwa na hali hiyo.Straika huyo ambaye alifunga mabao
sita katika mechi tatu za kwanza za msimu uliopita, safari hii amefunga
bao moja kwenye michezo mitatu aliyocheza.
“Hali hiyo ya kutofunga inanisikitisha sana na kuninyima raha, lakini
hivyo ndivyo soka lilivyo na bado sijakata tamaa, naendelea kupambana
ili kuhakikisha makali ya msimu uliopita yanarejea,” alisema Tambwe.
“Yaani hata mimi nashangaa juu ya hilo na nimekuwa nikijiuliza
maswali mengi, jana haiwezi kuwa sawa na leo, lazima kutakuwa na
mabadiliko.”
Post a Comment