Tambwe: Yaani hata mimi nashangaa!

SIMBA ipo mkoani Mbeya kujiandaa kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, keshokutwa lakini straika wa Simba, Amissi Tambwe ametoa kauli ambayo inaweza kuwa bado inawaumiza vichwa mashabiki wengi wa timu hiyo.
Tambwe amelia kutokuwa na bahati msimu huu lakini akasema kuwa yeye mwenyewe anashangazwa na hali hiyo.Straika huyo ambaye alifunga mabao sita katika mechi tatu za kwanza za msimu uliopita, safari hii amefunga bao moja kwenye michezo mitatu aliyocheza.
“Hali hiyo ya kutofunga inanisikitisha sana na kuninyima raha, lakini hivyo ndivyo soka lilivyo na bado sijakata tamaa, naendelea kupambana ili kuhakikisha makali ya msimu uliopita yanarejea,” alisema Tambwe.
“Yaani hata mimi nashangaa juu ya hilo na nimekuwa nikijiuliza maswali mengi, jana haiwezi kuwa sawa na leo, lazima kutakuwa na mabadiliko.”

Post a Comment

أحدث أقدم