KOCHA
wa Makipa wa Klabu ya Simba, Zdravco Djekic, amesema foleni za Dar es
Salaam zimekuwa zikimchosha na kumchanganya akili akihofia kuchelewa
kushindwa kukamilisha programu zake za mazoezi.
Kocha huyo mgeni nchini, ni raia wa Serbia aliyekulia Afrika Kusini,
amekuwa akiinoa Simba tangu Oktoba 10, mwaka huu wakati Simba
ilipokwenda Afrika Kusini.
Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha huyo alisema hajawahi kuishi
kwenye jiji lenye foleni kama Dar, hivyo kukaa kwa muda mrefu kwenye
foleni kunamfanya achoke na kumvuruga akili kitu ambacho siyo kizuri kwa
kocha.
“Foleni za Dar zinanitisha sana, naogopa nisije siku nikafika wakati
muda wa kumaliza mazoezi umefika. Tunakaa sana barabarani hadi mtu
unachoka, ikiwa nitaishi karibu na uwanja wetu tunaofanyia mazoezi
nitafurahi sana,” alisema Djekic.
إرسال تعليق