Tibaijuka asisitiza ushirikiano duniani kukabili changamoto mbalimbali


IMG_3160
Baadhi ya wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakiwapokea wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Na Mwandishi wetu
Tanzania imetaka jumuiya za kimataifa na washirika wa maendeleo kuhakikisha wanashirikiana na Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN)  yanafikiwa.
Umoja wa Mataifa ulianzishwa miaka 69 iliyopita kuhakikisha amani, maendeleo na ukuaji wa demokrasia ili kuifanya dunia hii kuwa mahali bora pa kuishi.
Kauli ya Tanzania imetolewa kupitia Waziri wake wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka mwishoni mwa wiki wakati wa kilele cha sherehe za miaka 69 ya Umoja wa Umoja.
Alisema hayo katika hafla ya mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya UN iliyofanyika jijini dar es salaam.
Alisema jukumu la Umoja wa Mataifa la kuwezesha maisha bora duniani haliwezi kufanikiwa kama kusipokuwapo ushirikiano wa dhati wa kukomesha changamoto zinazokabili dunia hii kama umaskini uliokithiri, ugaidi na magonjwa.
IMG_3187
Alisema kwa miongo mitatu Umoja wa Mataifa umejituma katika kutekeleza wajibu wake hasa katika kuleta usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira, kuelekeza maendeleo ya pamoja na kuhakikisha amani inapatikana.
Alisema mikutano mbalimbali ya kimataifa iliyofanyika kama ile ya Stockholm, Vancuva, Beijing ililenga kuweka msimamo wa pamoja ambao unawezesha dunia kuwa mahali pa amani ambapo mataifa yanashirikiana kuiweka salama dunia, kwa kuangalia changamoto za demokrasia,mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa binadamu huku suala la wanawake na watoto likitiliwa maanani.
Alisema juhudi za Umoja wa Mataifa umewezesha mabadiliko makubwa kuwepo ambapo dunia kama moja inafanya juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika maendeleo, kuwa na sauti moja katika kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo vita na magonjwa.
Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za afya, amani na maendeleo na kuleta usawa wa jinsia na  kushughulikia afya na maendeleo ya wanawake na demokrasia, bado UN ina changamoto kubwa inayoambatana na maendeleo yaliyopo.
Alisema umaskini uliokithiri na ugaidi umekuwa chanzo kipya cha migogoro inayotishia amani na  maendeleo ya dunia. Alizitaka nchi wanachama kuungana kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinatokomezwa.
IMG_3219
Akimkaribisha Waziri Tibaijuka kuongea Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, alisema kwamba wamefurahishwa na hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kutekeleza malengo ya milenia na kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kwamba malengo yale ambayo hayakufikiwa yanafanyiwa kazi katika mpango wa maendeleo ujao.
Aidha alishukuru Tanzania kwa kuipatia UN eneo la kujenga makazi kwa ajili ya mashirika yake yanayofanyakazi nchini .
Pia alisema kwamba wakati Umoja wa Mataifa unajikita katika kufanikisha maisha bora kwa wakazi wa duniani, inatambua changamoto zake zilizopo sasa ambapo mamilioni ya wananchi wanateseka kwa kunyonywa, usafirishaji haramu wa watu na kufanyishwa utumwa wa kingono.
IMG_3179
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke wakati wa zoezi la kupokea wageni kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Alisema ili kuwa na maendeleo na haki ni lengo la Umoja wa Mataifa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo ya kubadili dunia kuwa mahali bora pa kuishi.
Alisema wakati mpango wa malengo ya milenia unaisha mwakani ni vyema mataifa yakaendelea kufikiria kutekeleza yale ambayo haya kuwezekana katika agenda zao za maendeleo.
Alisema amefurahishwa na kauli ya serikali ya Tanzania kwamba imejipanga kuhakikisha inadhibiti ugonjwa wa Ebola na pia kuandaa mipango kwa vijana kupata ajira na kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha katika hotuba yake amesema kwamba kwa kuzingatia kwamba nguvu kazi kubwa sasa ni vijana ni vyema jamii ikaacha vijana waongoze kwa kuwa wao ndio wazazi wa kesho na pia ndio nguvu inayotakiwa katika ubunifu na uendeshaji wa shughuli za maendeleo.
Aidha alisema jumuiya ya kimataifa ni lazima itambue ushirikiano kama njia pekee ya kukabiliana na changamoto za dunia kwani hakuna nchi moja inayoweza kufanya shughuli yoyote peke yake.
IMG_3201
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka wakati wa zoezi la kukaribisha wageni kwenye hafla mchapalo ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
IMG_3211
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (waliyeshikana mkono) kwenye hafla mchapalo iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 69 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
IMG_3250
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman mara baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
IMG_3252
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akiwasili kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0029
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
IMG_3255
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati hafla hiyo ikiendelea.
DSC_0036
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka kuzungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
DSC_0060
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha malengo ya milenia yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
DSC_0062
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya “cheers” ya kuutakia kheri Umoja huo.
DSC_0074
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass “Cheers” kuutakia kheri Umoja huo kwa kutimiza miaka 69.
IMG_3257
Pichani juu na chini baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo mabalozi na wadau wa taasisi mbalimba za serikali na zisizoza kiserikali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar mwishoni mwa juma.
IMG_3258
IMG_3271
Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo.
IMG_3290
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
IMG_3379
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_3292
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bi. Jacqueline Maleko kwenye hafla hiyo.
DSC_0131
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi.
IMG_3385
Mkurugenzi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) akifurahi pamoja na wafanyakazi wenzake kwenye hafla hiyo.
IMG_3380
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka akifurahi jambo kwenye hafla hiyo.
IMG_3346
 Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakifurahi pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha CLOUDS FM, Barbara Hassan kwenye hafla  mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3337
Delivering as One… Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakipozi kwa picha na tabasamu bashasha la kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake. Kushoto ni Beatrice Mkiramweni kutoka ofisi za Mratibu Mkazi wa UN Tanzania na Msaidizi wa Mkurugenzi mkazi wa UNDP Tanzania, Eva Ruhago.
IMG_3321
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi, akibadilishana mawazo na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3342
Wadau wakiendelea kubadilishana mawazo.
IMG_3406
Selemani Kitenge kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi (kulia) akiwa amejumuika kwenye picha na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3367
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa mataifa na wageni waalikwa.
IMG_3317
IMG_3392
Tanzanite Band ikitoa burudani kwenye hafla mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya UN iliyofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
IMG_3430
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisakata rhumba na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Tonia Kandiero kwenye hafla mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar
IMG_3454
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimshukuru patna wake kwa kucheza muziki.
IMG_3444
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wageni waalikwa wakisakata muziki wa Live uliokuwa ukiporomoshwa na Bendi ya Tanzanite.
IMG_3440
DSC_0126
DSC_0128
Sawiche Wamunza (katikati) kutoka UNFPA akiwa na wafanyakazi wenzake.
DSC_0132
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiendelea kufurahia sherehe za miaka 69 ya Umoja wa Maitafa.
IMG_3459
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa Umoja wa mataifa na wageni waalikwa wakicheza “Kwaito” kwenye hafla mchapalo ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa mataifa.
IMG_3468
IMG_3478
Twende kazi….!
IMG_3486
Hapo sasa

Post a Comment

أحدث أقدم