Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa wa kwanza toka kulia pamoja na
Meneja wa duka hilo Irene Njovu na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania,lililopo Quality Centre
katika barabara ya Nyerere ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha
biashara jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi
wa duka jipya na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika
barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.Akimiminiwa kinywaji cha mvinyo
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)ikiwa ni moja
ya ishara ya uzinduzi wa duka hilo.Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto
ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam wakigonganisha glasi zenye mvinyo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa duka hilo. Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(katika) akiangalia moja ya Simu zinazouzwa katika duka jipya na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuzindua rasmi duka hilo kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kushoto kwa Meya ni Ofisa Mkuu wa Idara ya uuzaji na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh na kulia ni Mkuu wa Idara ya uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard.
Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania, lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katika
kuhakikisha wakazi wa Temeke na Ilala wanapata huduma kwa karibu,Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya katika jengo la
Quality Centre Uchumi lililopo katika barabara ya Nyerere ambalo ni
moja ya kituo kikubwa cha biashara jijini Dar es Salaam likiwa na maduka
makubwa,ukumbi wa sinema,sehemu za burudani na maofisi.
Duka hili
jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma
mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa Mpesa
na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa barabara ya
Nyerere,Keko,Ilala,Chang’ombe na Temeke kupata huduma kwa karibu.
Ofisa Mkuu wa
Idara ya Uuzaji na usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh,
alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya
Vodacom kuendeleza kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa
kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa
urahisi zaidi popote pale walipo.
“Uzoefu na
utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao
unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya
juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya
wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua
maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na
ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia”Anasema
Saleh.
Naye Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa,aliipongeza Vodacom kwa kufungua
duka katika eneo hilo lenye wananchi wengi na kuongeza kuwa anaamini
litawaokolea muda waliokuwa wanatumia kufuata huduma za Vodacom mbali na
kuwasihi kutumia huduma ya M Pesa kwani ni huduma iliyo bora na yenye
usalama zaidi.
Vodacom ina
mtandao wa maduka 82 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini
na duka lililofunguliwa leo ni la sita kufunguliwa katika wilaya ya
Temeke.Hivi karibuni inatarajia
إرسال تعليق