Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea kwa
msisitizo kuhusu maadili ya Utumishi wa Umma wakati wa ufunguzi wa mafunzo
elekezi kwa waajiriwa wapya wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya
Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas
Ndunguru akifafanua jambo wakati wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa
Wizara hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano uliopo Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mwajiriwa mpya katika kada ya Afisa
Habari akichangia mada wakati wa semina elekezi ya waajiriwa wapya wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo
elekezi kwa ajili ya kuwajengea uwezo kujua taratibu za Kiutumishi wa Umma
semina iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa wapya na baadhi ya viongozi wa wizara
hiyo mara baada ya kufungua mafunzo kwa watumishi wapya leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
إرسال تعليق