Mtu
mmoja amefariki mkoani Iringa baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira
waliojichukulia sheria mkononi kwa kuhusishwa na tuhuma za wizi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Isaya Mgimwa mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa maeneo ya Kinyanambo C wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa amefariki baada ya kupigwa na wananchi kwa kuhisiwa kufanya uhalifu.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu kujitafutia kipato kwa njia isiyo halali ambapo amefariki akiwa anaendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa
Aidha amewataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kutojihusisha na vitendo vya uhalifu pia watambue kuwa mahakama ndicho chombo kilichowekwa kisheria kwa kutoa hukumu kwa watuhumiwa hivyo wasijihusishe na vitendo vya kijichukulia sheria mkononi.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema jeshi la polisi mkoani Iringa linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wote walio husika na mauaji ya marehemu.
Post a Comment