
Watahiniwa binafsi wa mitihani ya kidato cha nne sasa watalazimika
kufanya mitihani miwili kwa kila somo ambapo mmoja utakua na alama 70
na wingine 30.
Meneja utawala wa Baraza la Mitihani la Taifa Daniel Mafie alisema
watahiniwa binafsi wamekua wakifanya mtihani mmoja ambao unachukua alama
zote 100 tofauti na watahiniwa kutoka shuleni ambao wao mtihani wa
mwisho una alama 70 na tathmini za maendeleo zina alama 30.
Alisema mfumo wa awali ulikua unawaumiza watahiniwa wa kujitegemea
ambapo kama mtihani wa mwisho ukiwa mgumu sana wengi wanafeli huku
wengine wakipata alama za tathmini za maendeleo.
Kwa upande mwingine NECTA imeweka utaratibu wa utoaji vyeti mbadala kwa waliopoteza vyeti vyao vya taaluma.
إرسال تعليق