Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akifungua kikao cha uhabarisho wa
chanjo mpya ya Surua na Rubella wilayani humo. Dc Mlozi pamoja na mambo
mengine, ameagiza viongozi wa madhehebu ya dini na wale wa kisiasa,
kushiriki kikamilifu zoezi hilo la kitaifa linalotarajiwa kuanza Okt. 18
hadi 24 mwaka huu. Jumla ya watoto 103,879 wilayani humo, wanatarajiwa
kupatiwa chanjo hiyo. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Singida, Mwendahasara Maganga.
Na Nathaniel Limu, Singida
SERIKALI
ya wilaya ya Singida, imewahimiza viongozi wa madhehebu ya dini na wa
kisiasa kutoa ushirikiano wa karibu wakati wa kampeni ya kitaifa ya
chanjo mpya ya Surua na Rubella inayotarajiwa kuanza Oktoba 18-24 mwaka
huu nchini kote.
Wito
huo umetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Queen Mlozi, wakati akifungua
semina ya uhabarisho juu ya chanjo hiyo, iiyohudhuriwa na kamati ya
uraghabishi na uhamasishaji wa jamii wilayani humo.
Alisema
Viongozi wa madhehebu ya dini na wale wa kisiasa, endapo watashiriki
kikamilifu, lengo la kuchanja watoto 103,879, wilayani humo,litafikiwa
kwa asilimia mia moja.
Mlozi
alisema zoezi hili ni tofauti na mazoezi yaliyopita, walengwa wa safari
hii ni kuanzia umri wa miezi tisa hadi chini ya miaka 15. Watapatiwa
chanjo mpya ya MR (Meales and Rubella).
Kwa
upande wake Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Singida, Emanuel
Mawi, alisema zoezi hilo litaambatana na utoaji dawa za vitamini A kwa
watoto wenye umri wa miezi sita hadi 59.
Mratibu
wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Singida, Emmanuel Mawi, akitoa mada
yake ya uhabarisho juu ya chanjo mpya ya Surua na Rubella inayotarajiwa
kuanza kutolewa kuanzia Okt. 18 hadi 24 mwaka huu nchini kote.
Alitaja
dawa zingine zitakazo tolea kuwa ni za minyoo (Mebendazole) kwa watoto
wa umri wa miezi 12 hadi 59, dawa ya minyoo (Albendazole) kwa watoto
wenye umri wa miaka 5 na kuendelea na dawa ya mabusha na matende.
Akisisaitiza,
alisema “Kwa kuwa baadhi ya walengwa wanapatikana shuleni, idaya ya
afya na idara ya elimu wilaya kwa pamoja zimeshiriki katika mafunzo, ya
namna zoezi litakavyokuwa na kuandaa mikakati ya kuhakikisha kuwa
walengwa wote wanafikiwa”.
Kuhusu
ugonjwa wa Rubella, Mawi alisema ugonjwa huo unaofanana sana na ugonjwa
wa surua,huwapata zaidi watoto walio na umri wa chini ya miaka 15.
“Mtoto
anapopatwa na ugonjwa huu, huweza kumsababishia matatizo mengi ikiwa ni
pamoja na ulemavu wa kudumu, upofu, utosikia, utindio wa ubongo, pia
endapo mama mjamzito atakuwa na vimelea vya ugonjwa huu, anakuwa na
uwezekano mkubwa wa kuzaa mtoto mfu, ama mwenye ulemamvu”, alisema Mawi.
Mkuu
wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi akifuatilia mada juu ya uhabarisho wa
chanjo mpya ya Surua na Rubella wakati kikao cha uhabarisho huo
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo. Wa pili
kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida,
Mwendahasara Maganga.
.Baadhi
ya wanakamati wa uraghabishi na uhamasishaji wa masuala ya chanjo mpya
ya surua na rubella wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa kwenye kikao
cha uhabarisho.(Picha na Nathaniel Limu).
Post a Comment