Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier, akihutubia katika hafla hiyo.
Dotto Mwaibale
TAKWIMU mbalimba za nchi zimetakiwa kutolewa na chombo chenye dhamana badala ya kutolewa kiholela jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya wakati akizindua Chapisho la Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/20012.
"Ni muhimu tafiti mbalimbali za maendeleo ya nchi zikatolewa na chombo chenye dhamana kwani kutolewa tofauti na chombo hicho zinaweza kuhatarisha maendeleo ya nchi" alisema Mkuya.
Katika hatua nyingine Mkuya alisema hali ya umaskini imeonekana kupungua nchini kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 kwa mwaka 2011/2012. Alisema chapisho hilo huwa linaisaidia Serikali katika kutathimini na kurekebisha baadhi ya sera na mipango ya maendeleo ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa nchi.
"Wakati nazindua chapisho hili inaonyesha kwamba kiasi cha sh. za Tanzania 36,482 kinahitajika katika kukidhi mahitaji ya msingi ya mtu mzima mmoja kwa mwezi ukilinganisha na kiasi cha cha sh. 19,201 kwa mahitaji ya aina hiyo ya mwaka 2007.
Alisema katika maeneo ya vijijini kiwango cha umaskini kimeonekana kupungua lakini hali hiyo imekuwa ni changamoto kwani asilimia kubwa ya watu wa vijijini wanatumia zana za kilimo za zamani.
"Utafiti unaonyesha kuwa kila watu 100 walikuwa na uwezo wa kufanya kazi mwaka 20011/12 watu 75 walijishighulisha na kilimo na uvuvi hata hivyo matumizi ya duni ya zana za kilimo bado imekuwa ni changamoto kubwa inayoedelea kutukabili,"alisema.
"Utafiti unaonyesha kwamba asilimia 96.5 ya kaya zinazojishughulisha na kilimo bado zinatumia jembe la mikono na asilimia 0.1 tu ndiyo zinatumia zana za kisasa za kilimo likiwemo jembe na plau na trekta. Aliongeza kuwa watu wengi hawana ushiriki wa benki katika shughuli za kibiashara wa ngazi ya kaya bado ni mdogo katika utoaji wa mitaji ya kuanzisha biashara katika ngazi hizo.
Alisema ni muda wa Serikali sasa kuweza kuwafahamisha hata kwa kuwapa wananchi njia za kujiari wenyewe ili kuweza kupunguza kabisa hali ya umaskini nchini.
إرسال تعليق