MAMA wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid (37) amejikuta akitelekezewa watoto hao na mumewe Matola, kisa akidai ni yeye tumbo lake kujaa maji. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Juni 12, mwaka huu, Ukonga-Mongolandege, Dar ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mume wake huyo lakini mara baada ya kuanza kwa dalili za ugonjwa huo mumewe alianza visa na kutoweka nyumbani.
Mama wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid aliyetelekezwa na mumewe kutokana na tumbo kujaa maji.
“Tulikuwa tukiishi vizuri lakini kutokana
na maradhi yaliyonikumba mume wangu aliamua kunikimbia na kunitelekezea
watoto hawa, sasa watoto wamekuwa ombaomba,’’alisema mwanamke huyo.
Hata hivyo, kufuatia na hali ya maisha yao kuendelea kuwa ngumu, nyumba hiyo waliyopanga walifukuzwa na kubaki wakitangatanga huku wakisaidiwa na majirani waliokuwa wakiwaonea huruma.Nyaraka za hospitali za Fatuma Ramadhani Rashid.
Alielezea kuwa watoto wake wameamua kuishi mitaani baada ya kushindwa
kwenda shule kwa kukosa ada ambapo mmoja wao alikuwa kidato cha kwanza
katika Shule ya Sekondari Mbuyuni- Chanika wilayani Ilala, Dar.Hata hivyo, kufuatia na hali ya maisha yao kuendelea kuwa ngumu, nyumba hiyo waliyopanga walifukuzwa na kubaki wakitangatanga huku wakisaidiwa na majirani waliokuwa wakiwaonea huruma.Nyaraka za hospitali za Fatuma Ramadhani Rashid.
Watoto watano aliotelekezewa Fatuma Ramadhani Rashid.
Mama huyo alisema kwa ugonjwa wake huo, alikwenda Hospitali ya Amana
na kuambiwa tumboni kumejaa maji lakini anaweza kutibiwa pasipo
kufanyiwa oparesheni ila anatakiwa kuwa na Sh. 500,000.Mama huyo aliomba yeyote atakayeguswa na tatizo la familia yake na yeye mwenyewe anaweza kumchangia kwa simu; 0783 521 182 Fatuma Ramadhani.
إرسال تعليق