Leo Novemba 22 taarifa ya habari iliyoripotiwa na kituo cha ITV
inahusu kuvuja kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG
kuhusiana na kashfa ya wizi wa fedha zaidi ya bilioni 300 kwenye akaunti
ya Escrow imekutwa inasambazwa mitaani.
Ripoti hiyo imekutwa ikiwa imetolewa
karatasi tatu za mwisho muhimu ambazo zina majina ya wahusika
waliogawana pesa hizo kwa lengo la kutengeneza propaganda ili
kuwadanganya wananchi kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika.
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia amesema; “…
imenyofolewa zile karatasi tatu ambazo ni muhimu zile za mwisho ambazo
ndio zinatoa hitmisho la uchafu wote uliofanyika.. Baada ya kutoa zile
kurasa tatu za mwisho, wakachukua taarifa hii kwa namna walivyoipata
wanajua wao wenyewe na kuanza kuisambaza kama njugu.. PAC wamejifungia
wanasema ni taarifa ya siri lakini taarifa iko mitaani.. Sisi kambi ya
upinzani Bungeni tumeona ni jambo baya sana, ni jambo ovu, ni jambo la
kifisadi, ni jambo la kishetani wanalotaka kuliingiza taifa letu liigie
kwenye machafuko kwa ajili ya maslahi ya watu wane, watano, sita, saba…
Baadhi ya watuhumiwa wameshakamatwa wako mikononi mwa jeshi la Polisi…”
Naye Mjumbe wa UKAWA John Mnyika amesema; “…
Rai yangu kwa Jeshi la Polisi watuhumiwa hawa ambao wamekamatwa na hasa
mmojawapo wa watuhumiwa ambaye naamini Jeshi la Polisi litapaswa
kumtaja kwa jina na kadhalika… Mimi ninazo taarifa kwamba mtuhumiwa huyu
ana mahusiano ya karibu na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo.. Kama mmoja wa watuhumiwa ana mahusiano na Sospeter Muhongo
ambaye ni mmoja wa watuhumiwa nahitaji vilevile Jeshi la Polisi
linapowahoji watuhumiwa waliokamatwa hasa huyo mtuhumiwa mmoja wao
lichunguze vilevile mahusiano ya mtuhumiwa huyo na Sospeter Muhongo …”
Katibu wa Bunge Thomas Kashirira na
Kamanda wa Polisi Dodoma wamesema wamesikia kuhusu taarifa hizo na
wanazifanyia kazi ili watoe taarifa rasmi.
Taarifa hiyo kutoka ITV iko hapa unaweza kuisikiliza.
إرسال تعليق