Ephraim Kibonde, Mussa Hussein, na wakali wengine wanaoisimamisha show ya Jahazi ya Clouds FM, leo kwenye ‘Mastori ya Town’ walikuwa wakipiga mastori na Diamond Platnumz
ambaye kaachia nyimbo mpya ya ‘Nitampata Wapi’ siku chache zilizopita,
na tayari imeonyesha dalili njema za kufanya vizuri baada ya kuanza
kupigwa na vituo vingi vya Redio na hata TV za kubwa Afrika kama MTV.
Sehemu ya mahojiano ya Diamond kwenye Jahazi iko hapa:-
Kibonde :- “.. Wanamuziki kila mmoja huwa anakaa upande wake, wewe umekaa kwenye mapenzi zaidi.. Kwanini kwenye mapenzi zaidi?…”
Diamond :- “…
Ukizungumzia mapenzi ni rahisi sana kuuza.. Hata ukiwa unazungumzia
suala la pesa lakini ukiingiza kwenye mapenzi tu basi zitauzika
kirahisi.. ndio maana nyimbo nyingi nikiimba nakuwa zinabase kwenye
mapenzi sana…”
Kibonde : “…Nyimbo
zako zimekwenda vizuri na umekwenda vizuri wakati wote, kuna nyimbo
nyingine ninayoipenda hii ya ‘Mdogomdogo’ ..Nini kilikufanya ukatoka
kule kwa mara nyingine tena kwa maana yake hapa ulihama hata kwenye zile
style zako za kubembeleza…”
Diamond: “…
Nilikuwa nimetoka kufanya Afropop halafu ilifanya vizuri sana, nikasema
nikifanya tena Afropop haitaleta ladha nzuri.. Nikaona mbona Wanigeria
wanafanya vya kwao sana, nikasema ngoja na mimi nichukue muziki wa kwetu
pia niujaribu kuumodify halafu nitietie njonjo ninazozijua mwenyewe za
kisasa hivi halafu ndo niutoe…
Kikubwa
ambacho kiukweli kilinipa moyo ni kwamba kulikuwa kuna tuzo zinafanyika
Marekani, imeingia kama nyimbo bora ya Kiafrika, ilikuwepo pia nyimbo ya
Davido, ‘Aye’ ilikuwepo nyimbo ya Bracket inaitwa ‘Mama Africa’ na
nyimbo zingine pia lakini katika nyimbo ambazo zilikuwepo ikaenda
kushinda hii kama nyimbo bora ya Kiafrika… Nikaona kumbe ukifanya hivi
inawezekana…”
Kusikiliza Mastori ya Town ya kwenye Jahazi la Leo, bonyeza play hapa kuisikiliza.
إرسال تعليق