Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe
waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza
wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa
Ripoti hiyo.
“…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa
watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa,
viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
“… Kamati
imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara
moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG
kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu alikuwa ana
taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota fedha kwenye
akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati za ofisi ya CAG ulionyesha
kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati
imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia
mhamala huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa
kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri
Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala
huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa
Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.
Kumsikiliza Zitto Kabwe akiwasilisha Ripoti hiyo, bonyeza play hapa.
Kumsikiliza Deo Filikunjombe akiwasilisha Ripoti hiyo, bonyeza play hapa.
إرسال تعليق