Abiria waliokuwa wanafanya safari na
shirika ka ndege la Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na
kuisukuma baada ya breki zake kuganda na kushindwa kuondoka.
Ndege
hiyo ilikuwa inaanza kuruka kutoka katika mji wa Kirusi wa
Igarka,lakini ilishindwa kusogea baada ya hali ya hewa kuwa -52C.
Abiria
waliokuwa ndani ya ndege hiyo idadi yao kubwa walikuwa wafanyakazi wa
ndege hiyo waliombwa kutoa msaada wa dharura wa kuisukuma ndege hiyo kwa
hofu ya kutowachelewesha endapo watasubiri msaada Zaidi.
Ndege
hiyo ya shirika la ndege la Katekavia baada ya muda ilimudu kuendelea na
safari zake na baadaye kutua salama katika mji wa Krasnoyarsk.kwa
muujibu wa mashuhuda wa tukio hili kiwango cha baridikwa muujibu wa
mashuhuda wa tukio hili ,wanaeleza kuwa kiwango cha baridi kilishuka
hadi kufikia nyuzi joto 52, na kugandisha mfumo wa breki za ndege hiyo .
Mkuu
wa kitengo cha huduma za ndege hiyo Oxana Gorbunova, anaeleza kwama
abiria hawakulazimishwa kuisukuma ndege hiyo bali kwa hiyari waliamua
kusaidia kuisukuma ,japokuwa kitendo hicho hakiruhusiwi kwakuwa kitendo
hicho kinaweza kuathiri bodi ya nje ya ndege hiyo ,na wanasheria nao
wanachunguza endapo uwanja wa ndege,shirika la ndege,wafanyakazi wa
ndege ama abiria endapo wamevunja sheria za usalama wa anga.
Uwanja
huo wa ndege unatumiwa na abiria takribani elfu moja kwa mwaka ,wengi
wao hufanya kazi katika makampuni ya mafuta yanayomilikiwa na Urusi.
- BBC
إرسال تعليق