![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRVbm9LlwzAxOYDKbagF3UtLirZegPwhryLB4DSWYTXLfXiRGBYX7HN0hjkltIazTH_eKpYw5KdJOXX8NW4LSBuJr-hlHkvmDmxvxBaIn0hgQ0ve_e4GWPrAwJSyWGaFlvChg5XXREkgs/s1600/MUSOMA+EXPRESS.jpg)
Basi
la Musoma Express lenye namba za usajili T138 BDQ lililokuwa likitokea
Dar es salaam kwenda Musoma limepata ajali majira ya saa 4 usiku katika
kijiji cha usanda shinyanga vijijini .
Basi hilo limepata ajali katika eneo la Usanda hatua chache baada ya kutoka katika mzani wa Tinde barabara ya Tinde Shinyanga.
Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamume mmoja anayedaiwa kuwa ni mzee (mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.
wakizungumza na
mmoja wa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga aliyeko katika eneo
la tukio,ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu yeye siyo
msemaji, amesema mwanamume aliyegongwa na gari hilo amefariki dunia
papo hapo na kwamba abiria waliokuwa kwenye basi hilo wako salama(hakuna
majeruhi wala waliopoteza maisha).
Walioshuhudia tukio hilo wameiambia kuwa dereva wa basi hilo hakuwa katika mwendo kasi ndiyo maana hakujatokea majanga zaidi.
Jeshi la polis
limefika katika eneo la tukio na ,Kamanda wa polisi mkoa wa
shinyanga Justus kamugishi amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo .na
kusema ni mtu moja mtembea kwa miguu alipoteza maisha hapo hapo. Mohab
Matukio
إرسال تعليق