Mtandao
wa Forbes umetoa list mpya ya matajiri hamsini kutoka Afrika list
ambayo inaongozwa na tajiri wa Nigeria ambae ni Mfanya biashara maarufu
na Rais wa kampuni ya Dangote Aliko Dangote, aliyekuwa akishikilia
nafasi ya arobaini na tatu na kupanda nafasi ishirini.
Forbes imetoa taarifa hiyo na kusema Dangote pia anashikiliana nafasi
ya hamsini na saba kwa watu matajiri Afrika na mtu wa pili katika watu
wenye ushawishi mkubwa.
Dangote ni mfanyabiasha mkubwa anaefanya biashara za Cement, Sukari,
Unga, Vinjwaji na biashara ya mafuta, bishara ambayo kwa sasa ina
thamani ya Dola Bilioni ishirini na tano pia ni mfanyabiashara mweusi
anayetajwa sana kati ya matajiri ishirini na tano Duniani.
Mmiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Globacom Chief Mike Adenuga, nae
ameingia katika nafasi ya pili ya matajiri Nigeria anaemiliki Dola
Bilioni nne nukta sita na kushikilia nafasi ya miatatu ishirini na tano
Duniani.
GENGE LAKIRI KUUA
WANAFUNZI 40 MEXICO
Mkuu wa sheria nchini Mexico anasema kuwa genge moja la wahalifu
limekiri kuwaua zaidi ya wanafunzi 40 ambao walitoweka wiki kadha
zilizopita.
Jesus Murillo alisema kuwa wanachama wa genge la madawa ya kulevya la
Guerreros Unidos linasema kuwa liliwaua wanafunzi hao na kisha likachoma
maiti zao.
Kundi hilo lilisema kuwa lilikabidhiwa wanafunzi hao na polisi baada ya
makabiliano kwenye mji wa Iguala.
Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa mabaki ya maiti hizo yamepatikana kando
ya mto na uchuguzi wa DNA utafanyika nchini Austria ili kuitambua.
Familia za wanafunzi hao zinasema kuwa zinaamini kuwa wanafunzi hao bado
wako hai.
Meya wa mji wa Iguala yuko kizuizini kufuatia kuwaamrisha polisi
kuingilia kati ili kuwazuia wanafunzi hao kuandamana
Make money by Copying: http://bit.ly/copy_win
Make money by Copying: http://bit.ly/copy_win
Post a Comment