
Makumbusho ya Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere yako hatarini
kutoweka kufuatia kusahaulika na serikali kushindwa kutoa fedha za
kuyahifadhi licha ya Mhasisi huyo kutoa mchango mkubwa wa kulikomboa
taifa na Bara la Afrika.
Akizungumza katika makumbusho ya hayati mwalimu julius kambarage
nyerere kijiji cha mwitongo wilaya ya Butiama mkoani mara muhifadhi wa
makumbusho hayo Baraka Bwire amesema anasikitishwa na serikali kutotoa
fedha za kutosha kuhudumia makumbusha ya baba wa taifa huku akisema kuwa
baadhi ya kumbukumbu zinaweza kutoweka kutokana na ukosefu wa vifaa na
mazingira Bora ya kutunzia kumbukumbu hizo.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati kuu ya chadema Grace Kiwelu
amesema ni aibu kwa serikali kushindwa kuyatunza makumbusho ya Baba wa
taifa na kubaki kumtaja kwa maneno huku makamu mwenyekiti wa Bawacha
Hawa Mwaifunga na naibu katibu mkuu Bawacha taifa Kunti Yusuph wameitaka
serikali kutumia rasilimiali alizoziacha Baba wa taifa kuboresha
makumbusho hayo ili yadumu kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo.
Baraza la wanawake wa Chadema Bawacha limetembelea makumbusho ya
hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuweka mashada ya maua kwenye
kaburi lake ikiwa ni ishara ya kumuenzi na kukumbuka mchango wake wa
kuimarisha umoja mshikamano na uadilifu katika taifa.
- ITV
Post a Comment