BREAKING NEWS:- BUNGE LAAHIRISHWA USIKU HUU BAADA YA VURUGU KUTOKEA

Kumetokea mtafaruku bungeni Dodoma baada ya kutokea mvutano miongoni wa wabunge kuhusu viongozi wanaopaswa kuwajibika kutokana na sakata la Escrow.

Baadhi ya wabunge hususani kutoak vyama vya upinzani wataka wahusika wawajibishwe ikiwemo kuachia ngazi,huku wale wabunge wanaodaiwa kuwa wa CCM wakionesha kutounga mkono maamuzi hayo huku wabunge wakidai wanawalinda baadhi ya viongozi.

Spika wa bunge Anne Makinda ameahirisha kikao cha Bunge hivi punde saa tano kasoro usiku huu,baada ya kutokea kwa  sintofahamu baada ya wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa.

Baadhi ya wabunge wamepiga kelele na kuimba bungeni, Spika ameahirisha bunge hadi watakaposhauriana

Post a Comment

Previous Post Next Post