Na Karoli Vinsent
HUKU ikiwa bado Jinamizi la ufisadi wa zaidi Bilioni 400
kwenye Akaunti ya Escrow likiwa bado lipo mikononi mwa Kamati ya Bunge
ya Hesabu ya Serikali PAC ili kuikagua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa
Serikali CAG kuhusu ufisadi huu,sasa Mazito yaibuka,MTANDAO HUU
UNARIPOTI.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu unazo zinaonyesha
jinsi watu mbalimbali walivyonufaika na ufisadi huo Mkubwa kuwai tokea
tangu nchi kupata Uhuru.
Watu hao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP
Engineering Bwana James Rugimalira ambayo kampuni yake ni mbia wa
Kampuni ya IPTL,ambapo taarifa hizo zinamuonyesha jinsi Bwana
Rugimalira akigawa mapesa ya walipa kodi wa taifa hovyo hovyo kama
hazina mwenyewe.
Waraka huu umekuwa ukisambazwa sasa ukionyesha alivyokuwa anagawana pesa hizo. |
Taarifa mbalimbali zinamuonyesha bwana Rugimalira ndiye
anayoitumia akaunti ya Banki ya Mkombozi na kuwagawa pesa kupitia
Akaunti yake ni 00120102523901 iliyoko Banki ya Mkombozi Jijini Dar Es
Salaam.
Rugimalira kampuni yake ya VP Engineering ndio ilikuwa
inamilikia hisa asilimia 30 na baada ya mgawanyo wa hisa hizo Rugimalira
alipata zaidi ya bilioni 98.
Chanzo hicho cha Kuaminika kinamuonyesha jinsi Mkurugenzi
huyo alivyowanufaisha marafiki zake hususani kabila la Wahaya kutoka
mkoani Bukoba.
Mhaya wa kwanza aliyetajwa na vyanzo mbali mbali ambaye
amenufaika na mgawanyo huo ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na
Makazi Profesa Anne Tibaijuka ambaye alipewa zaidi ya Bilioni 1.6 na
Rugimalira ambazo yeye Tibaijuka anasema alipewa kwa ajiri kuziokoa
shule zake.
Shule hizo Barbro Johanssen iliyoko Jijin Dar es Salaa na Kajumulu iliyoko Bukoba.
Mhaya Mwengine aliyenufaika na mapesa hayo ya Kifisadi ni Jaji
Aloysius Mujulizi ambaye naye alipewa Sh 40.4 milioni na Rugimalira.
Naye Prof Eudes Ruhangisa naye mhaya huyu kapewa Sh.404.2
milioni huku mipesa yote hiyo yawalipa kodi imepitia kwenye akaunti Na
00120102544301 katika benki ya Mkombozi.
Mtu mwingine kutoka Mkoa huo wa Bukoba ambaye naye ni pia Mhaya
ni Jaji Mujulizi ambaye naye alipewa mamilioni ya pesa kupitia kwenye
Akaunti Na 00110253580 kutoka benki ya Mkombozi
Neema
ya watu wa Bukoba kuvuna pesa za kifisadi ilienda pia kwa Bwana
Rweyongeza Afred Bitungwa ambaye naye alipewa na Rugimalira milioni 40
na alipotafutwa alikili kupewa pesa hizo na Rugimalira na kudai eti
alipewa kwa ajiri ya kusaidia matatizo madogodogo.
Mtu Mwingine ni bwana mmoja ambaye naye ni mhaya
alitambulika kwa jina moja la Kyabukoba naye alipewa kiasa cha pesa
ambacho bado mtandao huu unajakifahamu.
Wengine Jaji Ruangisa ambaye naye pia vyanzo mbalimbali vinamtaja kuwa lipewa mgawanyo huo
Zali hilo la kuvuna mipesa lilikwenda kwa Mhaya Mwingine ni
Rugozombwa Theophil ambaye ni mwanasheria wa RITA kupitia Akaunti Na
00120102602001,bwana Rugimalira alimuuingizia kiasi cha Milioni 323.4
milioni pasipo bila sababu yeyote fedha hizo ziliingia Februali 5 mwaka
huu
Akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM),
ilifunguliwa na mmoja wa wabia wa IPTL, James Rugemalira, ambaye
alikuwa akimiliki asilimia 30 ya IPTL huku kampuni ya Mechmar Bhd ya
Malaysia ikiwa na hisa asilimia 70.
Kutokana
na kiasi hicho cha hisa, Rugemalira amelipwa kiasi cha dola milioni 75
(Shilingi Bilioni 123), zikionyesha kwamba alilipwa kiasi cha dola
milioni 7.5 (Shilingi bilioni 12.4) mwaka jana na kiasi kilichosalia
alimaliziwa mwaka huu.
Kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa Rugemalira na kampuni ya
PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh, ambaye kwa sasa ndiye mmiliki
pekee wa IPTL baada ya kununua hisa za Mechmar na zile za VIP.
Akaunti hiyo ya Tegeta, ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi
fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya
pande hizo mbili umalizike.
Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya
Post a Comment