Imesema operesheni hiyo maalumu italenga kuuamsha
umma kutovumilia kashfa mbalimbali za wizi wa rasilimali za umma
zinazoibuka kila mara, lakini hatua stahiki hazichukuliwi.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara ya
Operesheni Delete CCM kwenye vijiji vya Hayderer na Luxmanda wilayani
Mbulu na Babati Mjini, naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum
Mwalimu aliwataka wananchi wa mijini na vijijini kujiandaa kwa
operesheni hiyo aliyosisitiza kuwa itasaidia kuwaondoa Watanzania katika
minyororo ya ufisadi unaozidi kuwafanya wawe maskini.
Mwalimu alisema haitoshi kwa viongozi kukiri
kuhusika au kulazimishwa kukubali ama kutolewa kafara ili kuiokoa
serikali ya CCM kila kunapotokea kashfa kubwa ya wizi wa fedha
zinazowanufaisha watu wachache na kuacha wengi wakifa kwa ‘njaa’, bali
nguvu ya umma inapaswa kutumika kuwaambia watawala kuwa “imetosha”.
“Naomba kutumia fursa hii ya mikutano, kutoa kauli
ya kuwataka Watanzania wenye uchungu na nchi yao kuwa tayari kwa
operesheni hii maalumu ambayo italenga kudai fedha zetu zinazoibiwa,
zikiwamo hizi za akauntin ya escrow,” alisema Mwalimu.
Kiongozi huyo alisema CCM inajua fedha zinazoibwa
serikalini zinakwenda wapi. Alidai kuwa mojawapo ya njia za kutafuta
fedha za kampeni za chama hicho ni kupitia kashfa za ufisadi,
akikumbusha wizi wa fedha za EPA zilizoporwa muda mfupi kabla ya kampeni
za Uchaguzi Mkuu wa 2005.
Mwalimu alikumbusha namna chama hicho
kilivyoshindwa kutekeleza mkakati wake wa kujivua gamba kwa maana ya
kufukuza wanachama mafisadi, lakini watuhumiwa wa ufisadi ndiyo viongozi
waandamizi hadi leo, wengine wakijigamba kuwa watakuwa wagombea wa
urais.
kupitia chama hicho.
Alisema CCM iliwalaghai Watanzania kwa kusema kuwa
ndani ya siku 90 kitaweza kuwashughulikia viongozi na makada hao lakini
hadi leo takriban miaka 4, kimeshindwa kuchukua hatua yoyote, akiongeza
kuwa badala yake ufisadi unazidi kuliangamiza taifa huku wananchi
wakitopea katika lindi la umaskini, maradhi na ujinga kwa kukosa huduma
za msingi za jamii ambazo ni wajibu wa serikali.
Alikumbushia pia kashfa ya ujangiri hususan mauaji
ya tembo ambayo yamekithiri kiasi cha kuichafua serikali kitaifa na
kimataifa, kuwa yapo majina ya baadhi ya viongozi wakubwa wa CCM
waliotuhumiwa kuhusika, lakini tangu walipotajwa kuhusika kwao, hakuna
hatua zozote zimechukuliwa. Ambo ambalo alisema linaonesha chama hicho
hakiwezi kutengana na ufisadi.
Alidai kuwa kila unapomalizika uchaguzi mmoja au
unapokaribia kumekuwa na ufisadi mkubwa wa mabilioni ya fedha,
unaofanyika serikalini kwa ajili ya kutafuta fedha kampeni na hususan
wanaotaka kuwania kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM.
…waliopewa zabuni hizo ambazo sasa zimegeuka kuwa
mwiba kwa wazalishaji wa ndani, ni sehemu ya mkakati wa kutafuta fedha
za kampeni,” alisema Mwalimu.
- Soma Zaidi Hapa(Mwananchi)
- Soma Zaidi Hapa(Mwananchi)
إرسال تعليق