Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Weka mbali na watoto! Prizenta asiyekaukiwa matukio wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ anadaiwa kutia aibu ukumbini baada ya kutaka kuzikunja na Master of Ceremony (MC) kisha kuumbuliwa na kigauni cha kihasarahasara alichokuwa ametupia.
Katika tukio hilo lililochukua nafasi kwenye Ukumbi wa White House mjini hapa, Dida alishuhudiwa akizama ukumbini humo akiwa mpole na mwenye kujificha kufuatia kuvaa kihasara lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo alivyokuwa akichangamka.
“Mh! Lakini naye Dida jamani kigauni gani kile kinaonesha hadi mambo ya ndani!” alisikika mmoja wa mashabiki wa Dida aliyekuwa ukumbini hapo.
Ili kuziba watu midomo, Dida alizama kwenye waleti yake akaibuka na ‘Misimbazi’ ambayo alimmwagia Warda na kuibua minong’ono kuwa yupo njema kimkwanja.
Kama hiyo haitosh i, mwanamama huyo alimfuata Meneja wa Planet FM, Anthony Muhando ‘Babu Bomba’ kisha akamkatia nyonga, jambo lililowashangaza wengi huku wengine wakipaza sauti wakisema ‘huyo ndo Dida wa…’ (hawakumalizia Dida wa nani).
Mwanahabari wetu alipomfuata Dida kujua kulikoni kuvaa kihasara na kucharuka kiasi hicho, bidada huyo hakutaka kutoa ushirikiano.
Weka mbali na watoto! Prizenta asiyekaukiwa matukio wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ anadaiwa kutia aibu ukumbini baada ya kutaka kuzikunja na Master of Ceremony (MC) kisha kuumbuliwa na kigauni cha kihasarahasara alichokuwa ametupia.
Prizenta asiyekaukiwa matukio wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’.
Tukio hilo lililoibua gumzo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye
shughuli ya ya kuzaliwa (birthday) ya shosti wake ambaye ni mtangazaji
wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani kupitia Kituo cha Redio Planet FM cha
mkoani hapa, Warda Makongwa.Katika tukio hilo lililochukua nafasi kwenye Ukumbi wa White House mjini hapa, Dida alishuhudiwa akizama ukumbini humo akiwa mpole na mwenye kujificha kufuatia kuvaa kihasara lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo alivyokuwa akichangamka.
Khadija Shaibu ‘Dida’ akijificha sura yake asipigwe picha na papalazi wetu.
Kuna wakati mtangazaji huyo alinyanyuka na kwenda kumvaa mwimbaji
nyota wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Amigo kisha akamgeuza na
kumkatia mauno kabla ya kutaka kushikana na MC Chuma aliyekuwa anaongoza
shughuli hiyo.“Mh! Lakini naye Dida jamani kigauni gani kile kinaonesha hadi mambo ya ndani!” alisikika mmoja wa mashabiki wa Dida aliyekuwa ukumbini hapo.

إرسال تعليق