DUDE SASA AGEUKIA MUZIKI

Stori: Gladness Mallya
NI sheeeda! Wimbi la wasanii wa filamu kuingia kwenye muziki limezidi kushika kasi ambapo muigizaji, Kulwa Kikumba ‘Dude’ naye ameamua kujitosa huko.

Muigizaji, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akistorisha na gazeti hili, Dude alisema ameamua kuingia kwenye muziki kwa kuvutiwa kwa muda mrefu na msanii Ambwene Yesaya ‘AY’ pia amewaona wenzake wanaoingia kwenye sanaa hiyo wakifanikiwa, hivyo naye anaamini atafanikiwa.
“Muziki ni kazi, nami nimeona ni vyema niwe na kazi mbili siyo vibaya hivyo kwa sasa nina wimbo mmoja ambao unajulikana kwa jina Bushi kwa Bibi, uko kwenye hatua za mwisho na nimeshautambulisha kwenye sherehe mbalimbali za wasanii wenzangu,” alisema.

Post a Comment

أحدث أقدم