Sakata linaloendela kati ya mshambuliaji star wa Totenham Emmanuel
Adebayor na mama yake mzazi anayefahamika kama Alice Adebayor
limechukua sura nyingine baada ya ndugu wa mshambuliaji huyo kuingilia
kati .
Ndugu huyo anayeitwa Kola Adebayor ambaye ni kaka wa Emmanuel
amesema kuwa madai ya mshambuliaji huyo ya kusema kuwa mama yao mzazi
amemroga si ya kweli.
Kola amesema kuwa kinachomfanya Adebayor kuamini kuwa mama yake
amemfanyizia kwa waganga ili asiwe na bahati ni mawazo anayoyapata toka
kwa watu wenye Imani ya dini ya kiislamu ambao wanamshauri vibaya nyota
huyo .
Kola mwenye umri wa miaka 42 ambaye kazi ni dereva wa Malorry huko
Ujerumani amesema kuwa amekerwa sana na kitendo cha mshambuliaji huyo
kumuita mama yao mzazi mchawi kwani inaonyesha jinsi gani alivyokosa
heshima kwa mzazi wake .
Kwa mujibu wa Kola , Adebayor aliwafuata watu wanaojiita
watakatishaji wa nafasi ambao kwa lugha ya kiingereza huitwa Spiritual
Cleansers ili wamsaidie kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri na kwa
mshangao mkubwa watu hao walimwambia kuwa mama yake mzazi na dada yake
ndio chanzo cha mikosi inayompata .
Kola anaendelea kusema kuwa Adebayor alifuata ushauri wa watu hawa na
kuwafukuza dada na mama yake kwenye nyumba aliyojenga huko Afrika na
tangu siku hiyo amegoma kuwatumia fedha za kujikimu .
Kwa upande mwingine dada wa Emmanuel Adebayor anayeitwa Maggie ndio
aliyefichua sakata hili huko Ghana wakati akizungumza moja kwa moja
kwenye kipindi cha radio ambapo alisema kuwa mchezaji huyo amemfukuza
mama yake na ametelekeza tangu siku hiyo .
Kola Adebayor anadai kuwa mama yao mzazi tangu siku aliyofukuzwa hadi
leo hii amekuwa akilia kila siku hali ambayo inahatarisha afya yake .
Mshambuliaji huyo amekanusha sakata hilo akisema kuwa sio kweli kuwa
amemfukuza mama yake bali mama huyo ameamua kuondoka yeye mwenyewe ,
Adebayor ameongeza kuwa hayuko kwenye mawasiliano mazuri na mama yake
kwani amekuwa akisambaza maneno kwa watu kuwa mambo hayatamwendea vizuri
.
Post a Comment