Habari wakuu,
Leo tunamaliza ngwe yetu ya mwisho bungeni, baada ya wasilisho la ripoti ya PAC, majibu ya serikali na mjadala wa wabunge wa jana, moja kwa moja kutoka Dodoma tuwe pamoja kuimaliza ngwe yetu. TANESCO wameshatoa tangazo rasmi la matatizo ya umeme hivyo chaji zetu ziwe vizuri nafasi ya kupata umeme inapopatikana.

=============

Spika ana Makinda ndiye aaliekalia kiti leo na Mwanri anajibu maswali yanayohusu wizara ya afya.

Mangungo(Nyongeza): Eneo la Mlandizi ni eneo la barabara kuu, nini ahadi serikali kuharakisha upatikanaji wa kituo ili kuwapelekea wananchi huduma karibu? Lipo tatizo la wahudumu wa afya na madaktari japo majengo yapo, nini jitihada ya serikali? Mwanri: Nakubaliana eneo la barabarani ajali nyingi, tutajitahidi kukamilisha haraka na kuona inafanyiwa kazi. Kuna vibali vimetoka kwa wahudumu wa afya pia wizara pia inapeleka watumishi moja kwa moja.
Tuliwapa nafasi cha watumishi 8,000 wizara ya afya pia tumewapa kibali cha watumishi 1,000 na bado hakijamaliza.

Suzan Lymo: Maslahi ya walimu lazima yaboreshe, serikali inafahamu tatizo Mwanri: Nakubaliana lazima kuboresha maslahi ya walimu, tuna upungufu wa walimu na nyumba za walimu. Mkakati wa serikali na pamoja na kudahili walimu na maabara, nyumba za walimu na kuimarisha mfumo wa kuwahudumia walimu.
Suzan Lymo: Kuna tatizo la upangaji walimu kwa shule za pembezoni, pia watendaji wanakaimisha walimu majukumu badala ya kukaa kwenye vituo vyao vya shule Mwanri: Kwanza kweli kuna tatizo, lakini tatizo kwa walimu wa sanaa limpembukua sana, tutafanya upangaji(re-allocation). Mwalimu kazi yake ni kufundisha hivyo kuwapa kazi za watendaji haikubaliki.
Leizer: Ni lini serikali itachukua mkakati kwa nyumba za walimu kama walivyofanya maabara! Mwanri: Jitihada za maabara tunazipongeza halmashauri, kuna halmashauri tumewapelekea milioni 500 kila moja ambazo zipo katika mazingira magumu.
===============

Maswali sasa ni kwa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo maswali yanajibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Stephen Masele.;
Mhe. Mbilinyi: Tunazungumzia sana mafanikio ya kusambaza umeme, kuna umuhimu gani wa kuendelea kusambaza umeme wakati huwa unakatwa kwenye nyakati maalum. Mfano; Jana kwenye mjadala wa Escrow?
Jibu: Tutofautishe kati ya kuwapatia umeme wananchi na kupatikana umeme wakati wote. Jana kulikuwa na hitilafu ndogo tu, ila Leo mbona umeme upo.
Mhe. John Komba (nyongeza)
: Katika Maeneo ya Mbamba bay, kwanini umeme mpaka sasa haujafika kama ilivyoahidiwa?

Jibu: Kuna Matatizo ya nguzo, kutokana na demand kuwa kubwa sana wakandarasi wameagiza nguzo za kutosha ili kuhakikisha miradi yote inakamilika.
Maswali kwa wizara hii bado yanaendelea....

============================== =========

Sasa ni zamu ya maswali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi;
Swali: Ni lini serikali itaboresha magereza kwa kuwa yapo kwenye hali mbaya kwa uchakavu, pamoja na miundombinu yake mibovu?
Jibu (Naibu waziri) : Serikali kupitia wizara yangu, ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hiyo.
Swali: Hivi karibuni, nchi jirani ya Kenya tukio la westgate lilitishia usalama wa nchi na raia wake, Je serikali imejipanga vipi kuzuia tukio kama lile lisiikumbe Tanzania?
Jibu: Tukio la Westgate la Kenya, lilikuwa ni tukio la kupangwa likihusisha masuala ya ugaidi. Serikali ya Tanzania kupitia jeshi la polisi, linajitahidi kwa makusudi kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuimarisha ulinzi.
==================

Maswali kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia;

Swali: Ni kiasi gani makampuni ya simu za mikononi zimelipa Kodi kwa Mwaka uliopita?
Jibu: Makampuni ya simu hulipa kodi kwa utaratibu uliowekwa. Aina za kodi ni pamoja na VAT, Service, Corporate TAX na nyinginezo.
Swali Nyongeza:
Hivi karibuni serikali imeweka mtambo wa kudhibiti simu zinazoingia na kutoka nchini. Je, imeongeza vipi kodi (pato)?

Jibu: Ni kweli serikali imeweka mtambo wa mawasiliano pale TCRA, Mtambo huo una kazi zake mbali mbali. Lakini kwa sasa serikali imefikiria namna ya kupata solution ya kuangalia namna gani itakagua mobile money transfer ili kuweza kutoza kodi.
Swali nyongeza (Zungu): Mheshimiwa waziri hujatoa majibu ya kitaalamu, kwani mtambo huo bado kabisa haujaanza kufanya kazi kama inavyotakiwa kufanya. Sasa nauliza, ni lini software hii ya kutoza wafanya biashara hasa wa mitandao ya simu italetwa na kuanza kufanya kazi ili mwananchi ajue kodi yake inaenda serikalini moja kwa moja?
Jibu: Kwa sasa mtambo unafanya kazi ya kukagua simu zinazoingia na kutoka, za kihalifu pamoja na kukagua mawasiliano kwa ujumla. ILa Tunaamini mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu kazi hiyo itakuwa imekamilika.
===================

Maswali na Majibu kwa Wizara ya Fedha;
Swali (Prof Makyusa): Tangu kuanzishwa kwa VICOBA wananchi wamenufaika sana, Je Serikali inaitambua VICOBA kama ni mkombozi kwa wananchi vijijini?
Jibu (Mwigulu): VICOBA ni miongoni mwa taasisi ndogondogo za fedha zinazoanzishwa ili kutatua changamoto za kifedha kwa wananchi hususan wa vijijini. Taasisi hizi husimamiwa na wananchi wenyewe. VICOBA si taasisi ya Serikali, bali ni ya mtu binafsi. Kwahiyo wizara haina bajeti kwa taasisi ya VICOBA.
Swali la Nyongeza: Kwa kuwa VICOBA si taasisi ya serikali na serikali haina bajeti kwa ajili ya taasisi hizi ndogo ndogo, Kwanini sasa isifikirie namna ya kuboresha na kuziwezesha hizi taasisi za microfinance kwa kuwa ni jambo jema?
Jibu: Serikali itajitahidi kupitia miradi ya maendeleo, kufikiria namna ya kuweza kuwezesha VICOBA, pamoja na kutoa mafunzo kwa wananchi wanaoishiriki kwenye VICOBA, Serikali pia inafikiria kuifanya VICOBA hatimaye kuwa rasmi kama hatua kubwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kujitegemea.
=========================

Ni zamu ya Maswali kwa Wizara ya Kilimo na Chakula;
Maswali yanaulizwa kuhusu kukosekana kwa pembejeo katika baadhi ya vijiji na wilaya, Na Wizara inajibu kuwa zoezi la kutoa pembejeo limeanza, labda Mawakala wanafanya zinachelewa kuwafikia wananchi, Hata hivyo wizara inadai itafuatilia.
============================== ====

Maswali kwa Wizara ya Maji;
Swali (Mhe. Mbilinyi): Tatizo la kukatika kwa maji na kukosekana katika maeneo mengi ya mbeya, linasabishwa na nini?

Jibu: Kukatika maji kunasababishwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara. Hivyo ni changamoto ambayo inafanyiwa kazi.

Swali la nyongeza:
Kuna tatizo la bili pia. Wananchi wanalalamika bili ya maji huja kwa bei ya juu tofauti na malipo ambayo hufanywa mara zote.

Jibu: Swala la bili huwa inatokea. Tutaliangalia hilo kwa umakini mkubwa.
============================== =

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi;

Swali (Nyangwine): Lugha ni nyenzo muhimu katika kujifunza, kwanini lugha ya kiswahili isitumike kama nyenzo rasmi ya kujifunzia?
Jibu: Lugha ya Kiswahili na kiingereza zinatumika kwenye kujifunza, hata hivyo suala hilo litapewa kipaumbele kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya kipekee.

Maswali machache yanafuatia. Majibu yanatolewa.

================
Mwisho ni Maswali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi;
Maswali yanaulizwa kuhusu sheria ya ardhi inayozungumzia ulipwaji wa fidia kwa wakazi wanaoathiriwa na uchimbaji au matumizi makubwa ya ardhi kwa maeneo husika. Ikiwemo kuwapa makazi mapya pamoja na fidia kulingana na thamani ya bei husika.
Wizara inajibu kuwa ni kweli, na sheria iko wazi. Isipokuwa kipengele cha ujenzi wa makazi mapya hakikuandikwa kwenye sheria lakini ni jambo la kufanyiwa marekebisho tu.

============================== ==============

UTAMBULISHO WA WAGENI NA MATANGAZO YA KAZI

============================== ==============

Mkono ameomba kuwa kwenye sehemu ya wachangiaji baada ya Muhongo kumuhusisha jana.

MJADALA

Nchambi: Anailaumu serikali kwa kuchelewesha kuleta jambo husika bungeni, watanzania wana hamu ya kujua fedha ni nani? Wakili wa TANESCO(Mkono) alishauri kufunguliwa akaunti(ananukuu maandiko ya biblia kuhusu kuheshimu mamlaka), anasema kila mtu atawajibika kwa namna yake.
Hasara nyingine tuliyoipta ni gharama za mawakili(bilioni 62) ambayo watuwengi hawaigusii, kesi imeenda miaka kumi hivyo haki kupatika ilionekana ni ngumi na bado tunadaiwa. Baada ya malipo tutakuwa tumepoteza bilioni 90 kwenye kesi.

Lazima tuangalie pande zote mbili, sehemu serikali inapotakiwa kuwajibika pia watu binafsi watatakiwa kuwajibika, fedha baada ya kutoka escrow na maamuzi(ruling) kutoka. Ilionekana bado TANESCO bado ingedaiwa lakini lazima serikali ituletee majibu dhidi ya mgogoro wa capacity charges.

Wizara ya nishati na madini ilikuwa na matatizo mengi kabla ya Prof Muhongo, tunapojadili hoja tujadili yenye mashiko. Tanzania ina kata 3804, Muhongo ameingia katika bajeti moja na kusambaza umeme vijiji vingi (ananukuu Quraan kuhusu kusema kweli).

Ananukuu Biblia watu wasiwe wakorofi(kumuingilia wakati anaongea), fedha za Escrow sio ugomvi ya ubadhilifu wa fedha pekee. Bei ya umeme tunaouziwa imeshika baada ya Muhongo, anasema kunaweza kuwa na chuki ya kibiashara hivyo tutumike kwa masilahi ya nchi na sio wafanyabiashara.

Kuwatisha wawekezaji sio jambo jema na tutapoteza imani na wawekezaji, waliotajwa kuhusika na fedha hizo serikali iwachunguze. Wapo watu wameingiziwa fedha kwenye akauti zao. Ananukuu Quraan kuhusu haki na batili, anapata mashaka mbunge kwenda kukagua wakati yeye pia anatiliwa mashaka. Kuna list ya watu itakuja hapa bungeni, kuna watu wa kambi ya pili wametetea hili jambo kwa upole na unyonge. Wabunge tusimamie haki na tuseme ya kweli, tulianza na Mungu na tuendelee na Mungu. Anamsifu Muhongo kwa kazi anayoifanya wizarani. Waziri mkuu ametajwa, ametajwa kwa namna tofauti na kuna watu ni majeruhi. Ananukuu Quraan kuhusu wajuzi, niwatie moyo mjadala uende vizuri.

Mwigulu Nchemba: Ukububwa wa jambo tunaongelea maadili na maslahi ya watanzania, nitajikita eneo linalogusa wizara ya fedha. Nazipongeza taasisi zote zilizoshiriki kwenye ripoti hii(anazitaja). Tangu utaratibu huu uanze, chimbuko la ripoti hii ni serikali yenyewe.
Kodi, imegawanyika maeneo matatu, VAT haikukatwa na kukatokea mkanganyiko, TRA inashughulikia na ni ilikua ni bilioni 26.97 lakini baada ya kugundua kuna kodi ya wananchi haijakusanywa ndipo wakakusanya bilioni 4.1 na ukaguzwa ni wa kwenye Escrow na sio IPT. Niwahakikishie watanzania kuwa kodi hii italipwa, hatuwezi kuacha kodi kwa tajiri halafu tukimbizane na mama mjane anaeuza mchicha barabarani.

Kodi ya pili ni iliyotokana na kukosewa kwa mahesabu na ni lazima ilipwe, TRA imeshaandika barua ya Novemba 2014 ya kufuta cheti(certificate). Brela wameshapewa notice ya kufuta capital gain certificate iliyotolewa kipindi kilichopita. Hatua imechukuliwa na serikali na tuko makini. Kuna watu wasio waaminifu, kuna mtu badala ya kuandika $ milioni 6 akaandika Tshs milioni 6 na badala ya kuandika $milioni 20 ameandika Tshs 20. Naagiza mamlaka ya TRA ifanye uwajibishaji wa ndani na akafanye kazi nyingi na hakuna uchunguzi juu ya uchunguzi. Mtu aliyeiba ukimfukuza kazi ni kumpa likizo akatumie fedha alizoiba hivyo mamlaka husika wachukue hatua. Tumeambiwa kuhusu pesa zilizogawiwa, na wenyewe walipie kodi kabla ya tarehe 31/12/2014. Baada ya tarehe hio TRA wafatilieni mmoja mmoja. Kuna taarifa pesa zilitoka kwenye mafurushi na magunia, nimefatilia na wamefata sheria. Anatoa agizo kwa Stanbic na Mkombozi watoe matamko, wateja wao wana haki ya kujua reputation ya benki yao. Niwaombe wabunge, kuna kuongea na kuchukua hatua na watanzania wanasubiri kuchukua hatua. Tumekua tunawachukulia hatua wanasiasa lakini wataalamu waliosomeshwa kwa kodi hawajibiki popote.(Muda umeisha)

Kafulila: Benki ya stanbic wamemfukuza kazi aliefungua akauti ya PAP amefukuzwa kazi asharudi kwao Uganda hivyo hizi ni dalili kuwa kuna makosa yalifanyika ndo maana hatua zimechukuliwa.

Mnyaa:
Nampongeza Nchemba kwa kusimama katika ukweli, economic hitman ni kama Mafia, na washawahi kuziangusha nchi(anazitaji) na miradi mikubwa wanayohusika nayo ni kama ya umeme, tujiulize kama hawajaingia Tanzania. Nyaraka nyingi zilizothibitishwa akatoa mbunge kuzikanusha ni kosa, Muhongo anasema ana nyaraka muhimu kwannini hakuzipeleka kwa CAG, maadili ya viongozi ambayo katika maazimio ya Richmond yaliazimiwa. Mwanasheria wa RITA leo yupo katika IPTL na mgao. CAG anapinga wabunge kuwa wajumbe wa bodi, leo hii sio conflict of interest? Wahusika ni IPTL na TANESCO na BoT NI MSIMAMIZI.

Imekuwaje BOT kutuma pesa PAP badala ya IPTL, kwa nini imekiuka akouti ya Escrow.

Mchangiaji: Ni dhambi kudhania PAC ni chombo cha wapinzani, kama kuna mapungufu ni bora tuyarekebishe, wanaofanya haya wanakula na viongozi wetu wa juu. Katika hili wananchi wameathirika sana kutokana na balaa hili la overcharge. Haiwezekana watu kuchukua pesa za dhulma na sisi wanyonge kuzilipa. Hakuna yoyote aliye alie juu ya sheria, uwajibikaji ni la lazima. Mbona alijiuzulu kwa mzigo wa watu wengine kwakuwa walikuwa chini yake.
Ashumta Mshana: Kuna taarifa tatu, ya serikali, PAC na CAG ila ukisoma zote zimetofautiana hivyo kutufanya tusielewe vizuri, taarifa ya PAC ina mapungufu mengi. Mbowe ametajwa kupokea pesa lakini haijataja.
Taarifa: PAC inafanyia kazi taarifa ya CAG, hayo majina unayoyasema hayakuwepo.
Ashumta: Kwani mapendekezo ya PAC yapo kwenye taarifa ya CAG
Mwenyekiti: Si vizuri kutaja majina ambayo hayapo kwenye ripoti.
Ashumta: Benki ya Mkombozi pekee majina yake ndio yameletwa, tunataka na majina ya Stanbic. Waziri mkuu hawezi kuondoka, tunao uhakika mbele yetu. Ripoti ya CAG hakukuwepo kuwa Muhongo amehusika moja kwa moja.
Waziri wa nchi: Kwa mujibu wa kanuni, nasogeza muda wa bunge mpaka saa nane mchana.

Nkumba: Serikali lazima ichukue hatua, haiwezakini ukapewa bilioni na Lugemalila lazima aseme alitoa hizo fedha kwa ajili ya nini. Nimshukuru Lugemarira ametusaidia sana kumaliza hili jambo hili. Hata kama ni chama cha mapinduzi tuwashughulikie.
Sendeka: Hapa hamna uwajibikaji wa pamoja bali mtaje wahalifu, wahalifu lazima wabebe, hakuna majina ya watu kwenye mauzo, huhitaji akili kubwa kujua kuwa hapa kuna uhalifu, watu wamekwepa kodi bilioni 8.7 kwa watu kughushi, haihitaji upoteze muda, utajua hapa kuna utapeli tangu mwanzo, kusimama na kusema ofisi ya CAG ni uongo mtaiambia nini dunia kwamba vyombo vyetu vyetu tulivyoviweka ni uongo. Hii ni dhambi, watu wanaopata fadhila za wizara wanakaa kwenye kamati. Muhongo kafanya kazi ya udalali, watanzania ni vyema wakapata majibu kama ni kweli ama la, kwenye mkataba unamtaja mheshimiwa Muhongo(anaunukuu)
Muhongo anaomba taarifa kuwa anachosema Sendeka ni uongo na kilichoandikwa si lazima awe sahihi, niwahakikishie watanzania hakuna mwekezaji yeyote nchi hii ambae hajaja kuonana na mimi.

Zitto: Nyaraka za CAG zimekua verified lakini za Muhongo alizozitoa uongo, mkataba unasema walikutanishwa na Sendeka.

Sendeka: Nimesoma kwenye mkataba ambao pia uko ofisini kwako na wewe umeshiriki, profesa aliita nyaraka nilizozileta ni za kufungia maandazi, hakuna shaka kuwa Muhonga alikua dalali katika dili hili, nina uhakika miongoni walionufaika ni waliowezesha dili hili. Ingekuwa haunizidi umri ningesema ulichofanya ni ukuwadi. Kodi la ungezeko la mtaji kila mmoja anajua tulivyoibiwa, ushauri wa nwanasheria mkuu umekwepesha kodi nchi hii, tunamlinda kwa sababu gani, Muhongo na Maswi pia bodi ya TANESCO inabaki kwa sababu gani! Tulimwajibisha, waziri leo anapewa masaa mawili kuitetea serikali ambayo si ya serikali bali wake mwenyewe. Mlienda Kunduchi kugawana fedha kwa njaa. Isaidieni nchi hii, hamuwezi kukwepa kodi alafu mkaja kutetea. Mwisho tupige kura juu ya mambo haya. Hatujakokotoa na bado tukampa Lugemalira lakini alilipa mabilioni ya kodi wakatiSeth mmemuacha. Mkono mlimpa dili wenyewe na mwanasheria wa TANESCO mkamfukuza bila haya, mi naomba waziri mkuu arudishwe. Huitaji kuwa msomi kujua. (Muda umeisha)
Lekule: Mhe M/Kiti, Hili suala tusiliwekee utani. Tusilizungumze wala kulijadili kwa mzaha. Ni jambo zito tusilete siasa. Sio suala la CCM kuiba fedha za UKAWA wala kinyume chake bali ni suala la wizi wa fedha za Umma.

Kiwango cha fedha kilichoibiwa, ni kiasi kikubwa. Hatuwezi kusema hizi pesa sio za umma, maana kuna fedha za kodi, hata kama pesa ni za mashirika, lakini zina kodi ndani yake. Kwahiyo ni fedha za Umma kwa na namna moja ama nyingine.

Akaunti ya escrow imeingiliwa na wezi wa aina mbalimbali. Leo tutafute sumu ya kuwapa hawa wezi wa hizi fedha.

Mhe. M/kiti, haya mabilioni yaliyogawanywa utashangaa, hivi huyu tajiri aliyegawa hizi fedha,anataka nini kwa hawa watu wote hawa? Hata duniani kote haijawahi kutokea tajiri akagawa pesa kwa namna hii.

Hizi fedha ni za jasho lake kweli? Maana haitegemewi fedha za jasho lake kugawiwa kwa namna hii, Matarajio yake ni nini kutoka kwa hawa watu?

Mhe. M/kiti, TANESCO ni shirika la umma, kwahiyo kama kuna fedha za TANESCO humo ndani tuna haki ya kudai. Kama ikishindikana kutowawajibisha hawa waliohusika na wizi huu, basi ni bora waliotangulia kama wakina lowassa, ngeleja na wengineo waje tuwaombe radhi, Kwa sababu sioni tofauti ya hawa viongozi.

Kwa sababu sitegemi nipewe 1.6 bilioni bila kujiuliza, hizi fedha ni za nini?

Kwahiyo naomba uchunguzi ufanyike zaid. Mimi nawapongeza kamati ya PAC, wamefanya kazi nzurri na bunge tuige kamati hiyo. Naomba na kamati nyingine zitakazochaguliwa kufanya kazi kama hii waige mfano huu.

<<<<<<>>>

Lekule: Mhe M/kiti bado nasema, hii kazi tunayofanya tufanye kwa umoja bila kumuonea mtu na tusilindane tufanye kama inavyotakiwa..(Makofi)

Asante sana.

====================

Mwenyekiti wa bunge, Mussa A. Zungu anaahirisha kikao cha bunge hadi saa 10 badala ya saa kumi na moja jioni, ili wachangiaji wawe wengi na kupata muda wa kutosha.

Wachangiaji watakaoanza jioni ni;

- John Mnyika
- Halima Mdee
- Esther Bulaya.............na wengineo.

Asanteni.
==============


DONDOO MUHIMU KIKAO CHA JIONI

Kigwangalla:
Sijawahi kuona Profesa muongo kama Muhongo
Kigwangalla: Toka lini pesa za watu binafsi zikawekwa Benki Kuu?
Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini. Pesa zilizotolewa hazijalipwa kwa mmiliki halali wa IPTL, PAP sio wamiliki halali!. Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliingilia majukumu ya TRA ktk kukusanya kodi
Zitto: Nimekuwa na mgogoro na chama changu lkn kwenye hili wameniunga mkono, kwa mara ya kwanza nimehudhuria kikao cha UKAWA
Kuna baadhi ya wajumbe wanadai tumetumwa na Uingereza. Hakuna kinachonituma kufanya haya, ni uzalendo kwa nchi yangu

Mahakama ilikiri kuwa kweli tulikuwa overcharged; ikaamriwa yafanywe mahesabu upya!

Prof. Muhongo alisema anaheshimu mahakama za ndani. Jaji utamwa hakuwa anaamua kesi ya Escrow wala Capacity Charges

Jaji hakusema kokote kuwa toeni hela mkawape IPTL. Hakuna sehemu alikotaja kitu kama hicho

Kama TANESCO ina madeni makubwa na haina hela; Tanzania ina deni kiasi gani la Taifa? Basi tumeshauzwa!

Muhongo alikuta TANESCO ikiwa na hasara ya Bil 43. Sasa TANESCO ina deni la zaidi mara 4!

TRA wamegundua fraud kwamba nyaraka za PAP zilikuwa forged! Nchemba ameonesha ukomavu ktk hili

Hivi watanzania tumefikia hatua ya kuukata utanzania kabisakabisa?

Prof. Muhongo anadai yeye hahusiki na mambo ya makampuni. Sheria iliyotungwa mwaka 2012 haisemi hivyo!

Umeme umekatika Bungeni, wabunge wanashangilia!
Zitto: Kijana aliyesema Singh ni tapeli ametengenezewa kesi ya mauaji. Alifukuzwa kazi! Naomba apatiwe ulinzi
Zitto: Prof. Tibaijuka aliniandikia mchango wake wa maandishi kuelezea alivyopata fedha; tunawaachua Kamati ya Maadili
Zitto: System ili-collapse wakati wa mchakato wa uhamishaji wa mabilioni haya
Zitto: Tuhuma zikiachwa bila kufanyiwa uchunguzi watu huziamini. Naomba tuhuma za Lusinde kwangu zifanyiwe uchunguzi
Zitto: Naomba wanaonishughulikia wanishughulikie mimi; mwacheni mamangu apumzike (anatokwa machozi)

Kafulila: Tusiache kujadili kifo cha Waziri Mgimwa kisa mwanae hataki; kuna siku Rais atakufa na mwanae atataka tusichunguze

Chenge: Naomba neno KUFA listumike bali litumike neno KUFARIKI linakuwa na staha kidogo

Pendekezo la Serikali kumkamata Harbinder Singh Sethi kwa money laundering limekataliwa na Serikali hadi kesi iliyopo iishe

Lissu: Sethi akamatwe. Shauri lililopo mahakamani ni shauri la baadae! Akamatwe kwa sababu jinai kubwa imefanyika
Lissu: Pendekezo hili la serikali naomba wabunge wasilikubali; mtu huyu ahukumiwe kwa jinai
Simbachawene anapendekeza Sethi asikamatwe kama ilivyopendelezwa na Serikali; wabunge wanazomea

Mdee: Si ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kesi ya jinai na kesi ya madai. Huyu Sethi afunguliwe kesi ya jinai
Halima Mdee: Kilicholetwa na Serikali ni ovyo, kinalinda wezi (kutaka Sethi asikamatwe mara moja)
Pindi Chana: Wa kukamatwa si Sethi peke yake; vyombo vya dola vifanye uchunguzi kwanza kubaini jinai iliyofanywa

Zitto: PCCB na TRA wameshafanya uchunguzi; mnataka vyombo gani vingine vifanye uchunguzi?

Werema: Eneo hili ndo litaleta mgongano mkubwa kati ya Bunge na Mahakama. Kwa sasa ni vigumu kusema "mkamate"

Makinda: Mnaposema akamatwe mnakosea, sisi siyo mahakama, tutafute njia nyingine na tuweke lugha ya kwetu siyo ya mahakama
==================


MAAZIMIO
Pendekezo la kwanza la kumkamata na kumfilisi bwana Seth lina marekebisho ya serikali, naibu waziri wa Sheria anasema haiwezekani
Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa

Azimio la TATU limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria
Pendekezo la NNE. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha
Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika

Azimio la TANO: Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo
Azimio la SITA: kuhusu Bodi ya TANESCO kuvunjwa kwa kusababisha pesa kuchotwa na hasara, serikali imekataa, mjadala unaendelea

Kingwangala: Kanuni zetu zinataka mtu yoyote anayetaka mabadiliko ya maazimio lazima awe amekawasilisha kabla
Kafulila: Kwa mujibu wa mkataba wa IPTL, maamuzi ya mwisho yanafanywa na mahakama ya London, bodi walikuwa na maamuzi hayo na haikuwajibika na maamuzi ya mahakama za ndani ya nchi
Majibu: ISCD ilisharidhia injuction ya mahakama ya Tanzania na ikaijulisha standard charted hivyo si sahihi kusema ISCD ina mamlaka ya mwisho, IPTL pia ilipata injuction kwenye mahakama za Tanzania
IPTL sio kampuni ya kimataifa tena bali kampuni ya ndani

Mdee: Bodi ya TANESCO, napendekeza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi vitendo vya jinai na kuchukua hatua kwa bodi ya TANESCO
Mbowe: Kazi yote hii pengine tusingefika hapa kama bodi ingekua makini, bodi ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama hii. Bodi ya TANESCO iwajibishwe
Lissu: Maneno ya Mdee yanahusu jinai, ishu ni bodi ya TANESCO, (Anapendekeza bunge livunje bodi ya TANESCO ivunjwe na iundwe upya kuongeze ufanisi.
Shekifu: Tusifike mahala bunge likatoa amri lakini kutekeleza shughuli pia tuna mihimili mitatu, bunge linaishauri tu serikali na bunge haliwezi kuivunja bodi ya TANESCO
Azimio hili ni la bunge hivyo tuepuke kuvunja katiba

Zitto: Bunge linaelekeza kwamba bodi ya TENESCO liundwe upya maana taasisi zote zimeshachunguza kama TAKUKURU na nyinginezo
Maelekezo ya Lissu yanapitishwa na wabunge

Azimio la Saba: Kamati imethibitisha katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini amefanya uzembe pia amesaidia pesa za Escrow akaunti kulipwa kwa asiyestahili, kamati inashauri uteuzi wake utenguliwe mara moja.

Waziri: Maswala yote yatachukuliwa hatua baada ya uchunguzi.

Kafulila: Halina mabadiliko na kama ni uchunguzi umeshafanywa na CAG na TAKUKURU, bunge kama chombo kinachoisamamia serikali libaki na meno yake ya kuisamamia serikali.
Simbachawene: Katibu mkuu ni mtumishi wa umma, na mwenye mamlaka nae ni raisi wa jamhuri hivyo bunge haliwezi.
Nagu: Nakubalianana uzito wa jambo, watendaji wa serikali wanawajibika kweli lakini wana haki zao, mamlaka husika waangalie na wachukue hatua.
Sendeka: Kamati inapendekeza uteuzi utenguliwe na TAKUKURU wamfikisha mahakamani, sisi tumeshauri na watu ambao tuna mamlaka nao ni waziri mkuu na raisi.
Zitto: Taarifa kwa waziri, taarifa hii inaweza kutumiwa na vyombo vya sheria.
Sakaya: Sio ikithibitika kwani kwa taarifa zilizopo imeshabitika
Suzan Lymo: Kwa uchunguzi ambao umeshafanyika, katibu mkuu huyu ana matatizo kwa sababu PAC na CAG ameshaonyesha
Vyombo vya kiuchunguzi viendelee kufanye uchunguzi

Lissu: Bunge litofautishe maswala la kijinai na mendine sio ya kijinai kama kutengua uteuzi. Wapo wanaolindwa na sheria, lakini wapo wanaoserve kwa mamlaka ya raisi hauwezi ukasema wana protection ya kisheria. Tunaomba nipendekeze bunge linaazima na sio kupendekeza.
Zitto anapendekeza katibu mkuu asimamishwe kupisha uchunguzi.
Wasira: Lazima tukubali nchi inaendeshwa na mihimili mitatu, juzi tulipata tatizo la mahakama kuzuia bunge na sisi pia bunge tusiingilie serikali.
Mchangiaji: Uchunguzi utafanyikaje wakati watu wako kazini?
Werema: Mimi ndiye niliyemshauri Katibu Mkuu Maswi kushughulikia fedha, ninambeba hivyo shughulikeni na mimi
Imeshindikana kupita kwa azimio la saba, Spika kaamua waendelee na azimio la nane, watarudi kupiga kura mwishoni.
Azimio la nane: Bunge limemuondoa Naibu Waziri wa Nishati Masele kwenye mapendekezo kwa kuwa hana hatia ya kuadhibiwa

Azimio la tisa: Linajadiliwa kuhusu kutengua uteuzi wa Waziri Prof Muhongo lakini upande wa serikali imekataa
Bunge halina mamlaka ya kumwambia raisi atengue baada ya Lissu kulitaka bunge kutengua uwaziri wa Muhongo.

Mbaruku: Bunge kazi yake ni kushauri na bunge haliwezi kuwa messenger. (Anashauri anavyoona)
Muhongo ameshutumiwa amedanganya bunge lakini hamna popote iliposemwa fedha hizi ni za umma moja kwa moja. Hivyo nashauri versin ya muheshimiwa Chenge.


Shaha: Tunachohitaji ni lugha nzuri bila kudharau muhimili mwingine. Tuhoji na tumalize na tuulize wanaoafiki Lissu au Chenge.
Zitto: Akili yangu imechoka kidogo hivyo sina pendekezo.
Mbowe: Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi.
Baadhi ya wabunge wanasema wezi waondoke...

Sendeka: Naomba tukae na tujenge hoja, (Kelele zinaendelea)

SPIKA ANAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MPAKA WASHAURIANE TENA(Spika aahirisha kikao cha Bunge ghafla baada ya kutokea sintofahamu baada ya Wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa )