
Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda
kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo
kipo ambapo amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.
Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na
Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni
kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili
amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya
hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa
mtoto huyo alikuwa akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.
CRD: KENGETE BLOG
Post a Comment