Mkurugenzi
Msaidizi Wizara ya Utamaduni, Michezo, Habari na Vijana Dkt. Kissui S.
Kissui akifungua Rasmi Kongamano la Ulingo wa Maendeleo ya Biashara na
Uchumi Karakana ya wajasiliamali uliofanyika Wazo Hill Tegeta, Katika
Hotuba yake aliwapongeza PSPF kwa kujitoa kuwasaidia wajasiliamali
kuwekeza kupitia Fao lao la Ujasiliamali na Kujiunga katika mfuko wa
uchangiaji wa Hiari wa PSS, Pia aliwapongeza Haiba Foundation kwa
kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo na Mwisho alitoa somo maalum kwa
ajili ya kuwasaidia wajasiliamali jinsi ya kupata Kipato na kujua
matumizi mazuri ya Fedha.
Afisa
Masoko kutoka PSPF Eliachi Remmy akitoa maelezo ya Kina juu ya Mfuko wa
Uchangiaji wa Hiari wa PSS ambapo alisema kuwa mfuko huu ni Ruhusa kuwa
mwanachama ukiwa raia au asiye raia wa Tanzania na anayefanya kazi nje
au ndani ya nchi pia kujiunga katika mfuko huu wa PSS ni Bure kabisa.
Aliongeza kuwa kama Mjasiliamali mfuko huu ni muhimu kwake kwa kuwa
anaweza kulipia kirahisi kabisa hata kupitia mitandao yote ya simu. Pia
alizungumzia kwa kina Mafai mbalimbali yanayopatikana PSPF kupitia
Mpango wa Hiari ikiwa ni pamoja Fao la Elimu, Fao la Ujasiliamali,Fao la
Uzeeni, Fao la kifo na Fao la Ugonjwa/ Ulemavu Mwisho aliwasisitiza
wajasiliamali kujuinga na mfuko huo wa PSS na kuwaeleza juu ya Mkopo wa
Nyumba.
Afisa
Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Michael Leon Kazimili
akizungumza kwa kina Faida za Kuwekeza PSS pia alitoa tofauti kati ya
Kuwekeza PSPF na katika mabenki na kusisitiza kuwa kuna faida kubwa kama
mtu akiwekeza katika Mifuko ya Jamii hasa PSPF kwamba kuna faida kubwa
ya asilimia 6% kama ukiwekeza PSPF, Pia alizungumzia mkopo wa nyumba
ambapo alisema kwamba Mwanachama wa PSPF awe ni wa Kuchangia kwa Lazima
au kwa Hiari atapata Mkopo wa Nyumba na atalipia kwa muda wa Miaka 25
kwa kuzingatia Taratibu za Mfuko.
Mwenyekiti wa Karakana ya Haiba
Foundation Mzee Adam Kaira akitoa utangulizi kwa wajasiliamali ambapo
alitoa mwelekeo wa Haiba Foundation pia alieleza kuwa kuna mpango wa
kuanzisha Benki ambayo itawasaidia wajasiliamali aliongeza kuwa mpaka
sasa Haiba Foudation imefanikiwa kuwa na vikundi 75 ambavyo vinafanya
vizuri, Pia aliongezea kuwa wajasiliamali wanaweza kupata Mkopo kuanzia
Tsh 400,000 hadi 1,000,000 na kuna wanachama walishapata, mwisho
alizungumzia juu ya wajasiliamali kuwekeza katika Mfuko wa Uchangiaji wa
Hiari wa PSS ambapo utawasaidia zaidi katika kuboresha maisha yake.
Mkurugenzi wa Haiba Foundation Adam
Ngamage akitoa mada juu ya Haiba ya Ujasiliamali ambapo alisisitiza
Jinsi gani Mjasiliamali anaweza kubadili mwenendo wake wa kuwa
mfanyabiashara mzuri na mbinu mbali mbali za kufanya Biashara yake iweze
kwenda mbele bila kukwama Mwisho alizungumzia umuhimu wa kuwekeza
kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga-Kuku Gren
Mushi Maarufu kwa Mama Kuku akizungumzia ujasiliamali lakini hasa huu wa
ufugaji wa Kuku ambapo yeye ni mzoefu wa muda mrefu na ameanza tangu
miaka ya 1970, alizungumzia jinsi gani wajasiliamali ambavyo wanaweza
kusaidiana katika njia mbalimbali, aliongeza amesisitiza Biashara ya
kuku sasa inakuwa sana na amesema kuna mpango wa kuanzisha Jokofu ya
kuuzia kuku ambayo yatakuwa katika maeneo mbalimbali yakiuza kuku kwa
vipande ili kila mwananchi anayehitaji kuku apate kitoweo hicho. Mwisho
aliwashukuru kwa Dhati PSPF kwa moyo wao wa Dhati
Muwezeshaji wa Kongamano hilo kutoka Haiba Foundation Chonya Libe akiendelea kutoa Mwongozo .
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa PSPF David
M. Mgaka akiwagawia Fomu za Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS
wajasiliamali wote waliofika katika Kongamano hilo.
Maafisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakifuatilia kwa makini Kongamano hilo la Wajasiliamali
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa Makini Kongamano hilo
Baadhi ya Washiriki wakijiunga na Mfuko wa kuchangia kwa Hiari wa PSS
Post a Comment