Hizi Ndio Sentensi 10 alizoongea Jaji Walioba zilizopelekea Vurugu Katika Mdaharo Leo

Jaji Warioba; "Tume ya Uchaguzi imalize kwanza kuandikisha wapiga kura baadaye ndipo ianze kutoa elimu, na baadaye Kampeni"

Jaji Warioba; "Rasimu ya Tume ilichukua mambo mengi mazuri kutoka katika Katiba ya 1977, haikuwa nia yetu kufuta kila kitu"  

Jaji Warioba; "Mambo yote mapya yaliyopendekezwa na Tume yamekataliwa na "  


Jaji Warioba; "Yamo mambo machache ndani ya Katiba inayopendekezwa, mfano ni malengo makuu kwa ufupi na haki za binadamu"

 Jaji Warioba; "Sehemu ya Haki za Binadamu pekee ndiyo ambayo imeboresha"

 Jaji Warioba; "Sehemu wanayosema imegusa makundi yote ni kwenye malengo lakini wameyaondolea nguvu ya kisheria"

 Jaji Warioba; "Katiba Inayopendekezwa haiweki uhakika wa 50 kwa 50 ndani ya Bunge, sisi tuliweka uhakika"

 Jaji Warioba; "Suala la mgombea binafsi limewekewa masharti magumu sana na hakuna mtu atakayeyaweza"

 Jaji Warioba; "Hiki walichokiweka kama Tunu, siyo Tunu bali ni Urithi, mfano ni Muungano, Muungano ni Urithi, siyo Tunu"

 Jaji Warioba; "Serikali ya Muungano itakuwa ni ya Tanganyika, na koti la muungano limekuwa kubwa zaidi"

Post a Comment

أحدث أقدم