Stori: DUSTAN SHEKIDELE , Morogoro ZAMANI kulikuwa na kasumba kwamba wanaume ndiyo huwapiga wanawake lakini hivi karibuni kibao kimegeuka ambapo mama mjasiriamali, aliyetajwa kwa jina moja la Mama Ashura ambaye ni mfanyabiashara wa viazi mviringo, anadaiwa kuwapa kipondo njemba watano kisa deni.
![](http://api.ning.com:80/files/dM6a4AYRwJOtZxN0j9x2n-uFZQ4mjcwjC01VJoabLDAxFqVcBZoJWxGeE-yMYBXgT2k3rHWwAda3Ppze648XtSex-ISmwO25/P1250924.jpg)
Baada ya zogo kuwa kubwa huku umati ukifurika eneo hilo, mmoja wa mashuhuda hao alimtonya mwanahabari wetu ambaye alifika fasta na kushuhudia mama huyo akipambana vilivyo na kundi la wanaume hao ambao aliwashinda nguvu kwa kuwashushia ngumi za kutosha.
![](http://api.ning.com:80/files/dM6a4AYRwJO7Xq0VL1qgtFEUgDP5aziG1GwS209r4VXMLC9URGCibcJg2zuIuY74X8vddo9OPKS-wZco-ZRrZXYfMzPAVAyF/P1250925.jpg)
“Kilichonifanya kuja hapa ni kwamba leo kaja sokoni kanunua gunia la viazi kwa mtu mwingine na akamlipa keshi hivyo nimeamua kumfuata anilipe deni langu.“Nimefika hapa anadai hana fedha, nimeamua kuchukua beseni lililojaa kuku na chipsi.”
![](http://api.ning.com:80/files/dM6a4AYRwJPPbOfJSmV9NhZKElGwAGJOZnjcE0xMl3ZEaOIfqWUk7BjgBv2efIG8Ijd20TRF1zJWq86Cnk5pmx6dk9FSc0tV/P1250927.jpg?width=650)
Kwa upande wa Babu alisema: “Nilipanga leo jioni nimlipe, cha ajabu kaja kufanya fujo ofisini, natafuta fedha nikamlipe maana kuku ni wa laki mbili na hili jua wataharibika.”
إرسال تعليق