Jaji Warioba ni shujaa hana sababu yoyote ya kuona aibu. Asikate tamaa bali tukio kama hili ndio liwe kichocheo kwake, kuweka juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi waielewe vizuri katiba inayopendekezwa, ili iwarahisishie kufanya uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura.
Viongozi wa vyama vya upinzani, fursa hizo
mnaongezewa kuwafikishia ujumbe wananchi. Mshindwe tu wenyewe kuufikisha
ujumbe huo kwa wenye nchi, halafu msiwageuke wananchi na kuanza
kuwalaumu kama ujumbe wenu hauwafikii ipasavyo.
Watanzania sio wapumbavu wala sio wajinga. Mwalimu
Nyerere alipozunguka nchi nzima kutafuta uhuru walimuelewa vizuri sana
na matokeo yake yalionekana.
Nyinyi pia nendeni kwa wananchi hao hao, waelezeni
yote upungufu uliopo waelewe. Wao pekee ndiyo wenye uamuzi wa mwisho.
Tumieni fursa hizi vizuri kuwaelimisha wananchi.
Edmund Charles,
Dar es Salaam.
Post a Comment