Jeshi la pamoja Afrika kukabili migogoro kuanzishwa

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jeshi la Pamoja la Afrika (AU) linalohusika na kukabiliana na migogoro na majanga barani Afrika ( ACIRC), Meja Jernerali Francis Okello (kushoto), akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo ya utulivu Afrika, jijini Dar es Salaam jana.PICHA: TRYPHONE MWEJI
Nchi 13 ambazo ni mwanachama wa umoja wa Afrika (AU) zimeanza rasmi maandalizi ya kuanzisha mpango wake wa kuwa na jeshi maalum  litakalokuwa tayari kukabiliana kwa haraka dhidi ya migogoro na majanga yanayojitokeza gafla (ACIRC), katika nchi hizo.
Hatua hiyo inafuatia makubaliano ya wakuu wa nchi hizo yaliyofikiwa katika kikao  cha Mei, mwaka huu  mjini Addis Ababa, Ethiopia pamoja na kile kilichofanyika Novemba, Afrika Kusini mwaka huu.

Mkuu wa Mafunzo wa ACIRC, Meja Jenerali Francis Okello, kutoka Jeshi la Wananchi wa Uganda (UPDF), alisema mpango huo unatarajia kuanza hivi karibuni baada ya kikao cha wakuu wa nchi hizo kitakachofanyika Ethiopia.

Alisema lengo la kuanzisha jeshi hilo ni kutaka nchi hizo ziwe na jeshi lake la uhakika linaloweza kupambana na majanga wakati wowote badala  ya kusubiri msaada kutoka nchi zilizoendelea.

Aliongeza kuwa tayari majeshi ya nchi hizo yamekutana jijini Dar es Salaam tangu Novemba 25, mwaka huu kwa ajili ya kupanga mikakati na mafunzo ya namna jeshi hilo litakavyoendeshwa.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم