Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani
anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise
Campaore baada ya miaka 27 uongozini.
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (katikati),akitangaza kuchukua madaraka kwa waandishi wa habari.
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati
kati),akizungumza kwenyemkutano na waandishi habari kutangaza kwamba
anachukua madaraka ya nchi akiwa katika makao makuu ya jeshi mjini
Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 31, 2014.
Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukaniBlaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.
Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa
kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida
iliyosema kuwa amechukua jukumu la kuliongoza taifa hilo.
Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (katikati),akitangaza kuchukua madaraka kwa waandishi wa habari. Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukaniBlaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.
(Chanzo: BBC)

Post a Comment