Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Instagram, bila shaka siku za
hivi karibuni hasa jana na leo umekuwa ukiona picha za mastaa kibao wa
Marekani wakiwa wamevaa nguo za ajabu ajabu na kuandika #Happy
Halloween!

Tunaamini umeona pia baadhi ya watanzania wakiwa wamevaa nguo za aina hiyo na kuandika kitu hicho hicho. Lakini bado ukweli ni kuwa watu wengi sana duniani hawafahamu maana na chimbuko la sikukuu hii.
Halloween ni miongoni mwa sikukuu kongwe zinazoendelea kusherehekewa hadi leo hii. Ni miongoni mwa sikukuu maarufu duniani, pengine ya pili baada ya Christmas.
Wakati mamilioni ya watu wanasherehekea Halloween bila kujua chimbuko lake, historia na ukweli wake, hufanya sikukuu hiyo ivutie zaidi. Baadhi ya watu huichukulia Halloween kama muda wa kufurahi, kuvaa nguo tofauti na kula bata kwa party za aina mbalimbali.
Wengine huiona kama muda wa masuala ya kishirikina, mizimu, mahoka na uchawi mwingine ambao unapaswa kuepukwa kwa gharama yoyote. Halloween pia ni sikukuu ambazo kwa dini kama ya kikristu zimeleta mkanganyiko kwa muda mrefu.
Historia ya Halloween
Halloween hufanyika kila October 31, siku ya mwisho ya kalenda ya Celtic. Awali siku hiyo ilikuwa ni siku ya wapagani kuwakumbuka waliokufa. Halloween ilikuwa ikimaanisha ‘All Hallows Eve’ na hiyo ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
All Hallows Eve hufanyika jioni kabla ya All Saints Day, iliyotengenezwa na Wakristo kuwabadilisha wapagani na husherehekewa November 1. Kanisa katoliki huwaenzi watakatifu wake katika siku hii.
Chimbuko la Halloween
Pamoja na kuwa na aina nyingi za machimbuko na mila za zamani, mengine yameendelea kubakia vilevile. Tamaduni tofauti huchukulia Halloween kwa aina tofauti lakini mila za Halloween zimebaki kuwa zilezile.
Utamaduni wa Halloween unakumbukwa enzi za Druids, utamaduni wa Celtic huko Ireland, Uingereza na Ulaya Kaskazini. Kulifanyika karamu ya Samhain, iliyokuwa kila mwkaa October 31 kuwakumbuka waliokufa. Samhain inamaanisha “summers end” yaani mwisho wa kiangazi au November.
Samhain ilikuwa ni sherehe ya mavuno na uchomaji wa moto kumaliza mwaka wa Celtic na kuanza mpya. Mambo mengi yaliyokuwa yakifanyika kwenye sherehe hizo yalihusiana na imani za kishirikina. Celts waliamini kuwa nafsi za waliokufa zilikuwa zikizunguka mitaani na vijijini usiku. Kwakuwa si mizimu yote ilikuwa ikiaminika kuwa salama, zawadi mbalimbali zilikuwa zikiweka nje kuituliza ile mibaya kuhakikisha mavuno ya msimu ujao yatakuwa mazuri.
Mila hiyo huhusisha trick-or-treating ambapo watoto huzunguka nyumba hadi nyumba kuomba kupewa vitu mbalimbali kama chakula nk.

Post a Comment