Rais Barrack Obama ataka kurudishwa mamlaka kwa raia nchini Burkina Faso
Marekani imelaani kile ilichokitaja kuwa mipango ya jeshi nchini
Burkina Faso ya kulazimisha inachotaka kwa watu raia kufuatia kujiuzulu
kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Jeshi limemteua kanali Isaac Zida kama kiongozi mpya wa serikali ya mpito.
Lakini
kwa upande wake Marekani inataka kuwepo utawala wa kiraia nchini
Burkina Faso mbali na mipango ya kuwepo kwa uchaguzi wa urais, wito
ambao pia ulitolewa na muungano wa Afrika.
Kanali Issac Zida ambaye ameteuliwa na jeshi kuongoza serikali ya Mpito ya Burkina Faso.
Kanali Issac Zida ambaye ameteuliwa na jeshi kuongoza serikali ya Mpito ya Burkina Faso.
Upinzani nchini Burkina Faso unasema kuwa hautakubali uongozi wa kijeshi na umeitisha maandamano leo Jumapili
Bwana Compaore ameikimbilia Ivory Coast baada ya kulazimishwa kuondoka madarakani kupitia maandamano.
Post a Comment