Listi
ya washiriki waliobaki ndani ya jumba la Big Brother Africa imezidi
kushuka tena leo, muda mfupi uliopita tumeshuhudia washiriki wengine
watatu wakitolewa ndani ya Jumba hilo.
Kutoka kwa washiriki Kacey Moore ambaye
alikuwa anawakilisha Ghana, Luis mwakilishi wa Namibia, na Arthur
mwakilishi wa Rwanda kumefanya idadi ya washiriki waliotoka mpaka sasa
kufikia washiriki kumi, wanne kati yao ni wa kiume na wa kike sita.
Hizi ni baadhi ya picha za matukio wakati washiriki hao wakiwa wanatolewa.

Arthur, mwakilishi wa Rwanda aliyetolewa BBA Hotshots.



Washiriki wa BBA waliotolewa, Kacey Moore (aliyevaa miwani)wa Ghana na Luis wa Namibia (Kulia).




إرسال تعليق