Wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wamefanya ziara ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata (km 64), inayojengwa
kwa kiwango cha lami. Barabara hii inaunganika na barabara kuu ya Dar
es salaa – Chalinze – Arusha katika eneo la Msata. Hivyo ni njia mbadala
ya kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kanda ya Kaskazini na nchi
jirani ya Kenya.
Barabara
hii inayojengwa na kampuni ya Estim Construction ltd, na kusimamiwa na
mhandisi mshauri kampuni ya JBG Gauff Ingenieure GMBH & Co.
Mkandarasi wa barabara hii ya Bagamoyo – Makofia – Msata anatarajia
kukabidhi barabara hii Machi, 2016.
Aidha,
kamati hiyo ilipata nafasi ya kutembelea mizani ya kisasa iliyopo eneo
la Vigwaza inayojengwa na kampuni ya M/S China Henan International
Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) na mhandisi mshauri kampuni ya
Ambicon Engineering Ltd of Tanzania.
Mradi
huu hadi sasa umekamilika kwa asilimia 95. Ikiwa ni kukamilika kwa
barabara ya maingilio, maegesho ya magari, majengo, ofisi, gereji na
jenereta, vyoo vya wasafiri pamoja na mizani.
Mradi
huu unakamilika Novemba 2014. Kwa habari zaidi tazama picha za ziara
hiyo.(Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini – Wizara ya
Ujenzi)
Naibu
waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge (Mb) akiwasili eneo la mradi
akiambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter
Serukamba.
Wajumbe
wa kamati ya bunge ya Miundombinu wakipata taarifa ya mradi wa ujenzi
wa barabara ya lami Bagamoyo – Makofia – Msata (Km 64) kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale.
Ramani ya mchoro ambao barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata itaungana na barabara ya Dar es salaam – Bagamoyo.
Mkandarasi Kampuni ya Estim Construction Ltd,akiendelea na kazi ya ujenzi wa barabara hiyo.
Daraja la kioga lililopo kwenye barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata lenye urefu wa meta 55 limekamilika ujenzi wake.
Mhe.
Gerson Lwenge naibu Waziri wa ujenzi aliyenyoosha mkono akitoa maelezo
ya ujenzi wa daraja kubwa la mto Ruvu chini lenye urefu wa meta 140 kwa
wajumbe wa kamati ya Miundombinu.
Wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wakionekana kwa mbali wakishuhudia
mtambo wa kuchimba mashimo kwa ajili ya ujenzi wa nguzo za daraja
ukifanya kazi eneo la mto Ruvu chini daraja hili litakuwa na urefu wa
meta 140.
Naibu
waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge pamoja na wajumbe wa kamati ya
Miundombinu wakiangalia eneo la mto Ruvu chini ambapo daraja litapita.
Msafara wa wajumbe wa kamati ukikagua barabara hiyo huku wakielekea mizani ya kisasa eneo la Vigwaza.
Wajumbe wa kamati ya Miundombinu wakipewa taarifa walipowasili eneo la mizani, Vigwaza.
Picha ya mizani ya Vigwaza ikionekana kwa mbali huku magari makubwa na madogo yakipishana.
Mtendaji
Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale akitoa taarifa ya maendeleo
ya ujenzi wa mizani ya kisasa eneo la Vigwaza wa wajumbe wa kamati ya
Miundombinu.
Post a Comment