
.Zipo
50 na nyingine zina sifa ya kipekee
.Yadaiwa
kuna upungufu wa fedha na waumini
.Kadinali
asema pamoja na huzuni lazima zifungwe
New
York, Marekani
ZAIDI
ya parokia 50 katika jimbo kuu la kanisa katoliki, New York nchini Marekani
zitafungwa katika kile kilichodaiwa na kanisa hilo kujikusuru na madeni ya
parokia zisizojiendesha.
Miongoni
mwa parokia ambazo zinatarajiwa kufungwa ni ile ya East Harlem, kanisa la
kwanza kuwakaribisha waumini kutoka Puerto Rico. Parokia nyingine ni ya Upper
East Side lilianzishwa kwa sadaka ya dola 50 kutoka kwa waumini wafanyakazi
kutoka Italia katika miaka ya 1920. Na kanisa pekee linaloendesha misa kwa
lugha ya kilatini kila siku lenye umri wa miaka 150 lililopo Midtown.
Aidha
imeelezwa kuwa mwaka ujao zaidi ya pariokia 50 pia zitafanyiwa marekebisho
makubwa ikiwa pamoja na kuunganishwa na parokia nyingine.
Ufungaji
huo wa makanisa haujawahi kutokea katika kipindi cha miaka 164 ya Jimbo kuu la
New York.
Mpango
wa kufunga makanisa ni sehemu ya mchakato wa kubadili sura na mwelekeo wa
kanisa la new York Kiutendaji ulioanza mwaka 2010.
Kwa
mujibu wa gazeti la New York Times makanisa yatakayofungwa yatatamkwa kesho
Jumapili.
Tayari
vuguvugu la upinzani dhidi ya hatua hiyo zimeanza hasa kw amakanisa ambayo
yanaonesha yapo katika hatari kw akutofikia vigezo vilivyowekwa na watawala.
Jimbo
kuu lina parokia 368 katika maeneo ya Bronx, Manhattan, kisiwa cha Staten
na kwenye kaunti saba zilizopo kaskazini mwa Jiji.
Mwaka
2007, kadinali Edward M. Egan alifunga parokia 21 na kuzua sokomoko kubwa
miongoni mwa waumini ambalo bado linaendelea katika baadhi ya parokia hizo.
“baadhi
ya waumini wetu watahuzunika,watachanganyikiwa na hata kukasirika,” Mrithi wa
kadinali Egan kama Askofu Mkuu,Kadinali Timothy M .Dolan aliandika katika
gazeti la wakatoliki wa New York kuhusiana na mabadiliko hayo.
Alisema
anaelewa kuhusu hali hiyo kwani wengi wa waumini wanatambua kwamba parokia hizo
ndio mama wa imani.Alisema wakatoliki wanathamini paroki zao na hilo litawauma
sana.
Imeelezwa
kuwa sababu za kufunga parokia hizo ni zile zile za mwaka 2007 ikiwamo ya
kupungua kwa idadi ya mapadri wa kuhudumia kartika parokia,tatizo la kifedha
kupungua kwa idadi ya wakatokliki wanaobatizwa na kuoa au kuolewa kanisani.
Dayosisi
ya Brooklyn ambayo hujumuisha na Queens, ilikabiliwa na tatizo hilo hilo
na kuchukua hatua za kufunga baadhi ya parokia zake kufikia 187
kutoka 199 kwa mwaka 2009.
“hatuna
fedha kila mwaka kutoa dola milioni 40 kusaidia parokia zisizohitajika,”
alisema Kadinali Dolan katika blogu yake mwaka jana.
Kwa
mujibu wa habari za ndani paroko wanaohusika na kufungwa kwa parokia zao
wameambiwa hali hiyo Ijumaa iliyopita na leo katika makanisa yote kutakuwa na
taarifa.
Mwaka
mmoja uliopita, wakishauriwa na watu kutoka nje waliajiriwa na kanisa,
walitembelea kila parokia ambapo waliomba ikusanye waumini wake kuangalia uwezo
wao na udhaifu wao na kujadiliana na parokia jirani kuhusu walichiokiona katika
majadiliano kuhusu parokia yao.
Baadaye
kamati za ushauri ambazo zilijumuisha mapadri na waumini wa kawaida zilipitia
taarifa hizo na kuzitolea mapendekezo Aprili mwaka huu.
Mapendekezo
hayo yalifika kwa kadinali Juni mwaka huu.
Post a Comment