Kanisa katoliki yafunga parokia zisizojiendesha

.Zipo 50 na nyingine zina sifa ya kipekee
.Yadaiwa kuna upungufu wa fedha na waumini
.Kadinali asema pamoja  na huzuni lazima zifungwe

New York, Marekani
ZAIDI ya parokia 50 katika jimbo kuu la kanisa katoliki, New York nchini Marekani zitafungwa katika kile kilichodaiwa na kanisa hilo kujikusuru na madeni ya parokia zisizojiendesha.
Miongoni mwa parokia ambazo zinatarajiwa kufungwa ni ile ya East Harlem, kanisa la kwanza kuwakaribisha waumini kutoka Puerto Rico. Parokia nyingine ni ya Upper East Side lilianzishwa kwa sadaka ya dola 50 kutoka kwa waumini wafanyakazi kutoka Italia katika miaka ya 1920. Na kanisa pekee linaloendesha misa kwa lugha ya kilatini kila siku lenye umri wa miaka 150 lililopo Midtown.
 Aidha  imeelezwa kuwa mwaka ujao zaidi ya pariokia 50 pia zitafanyiwa marekebisho makubwa ikiwa pamoja na kuunganishwa na parokia nyingine.
Ufungaji huo wa makanisa haujawahi kutokea katika kipindi cha miaka 164 ya Jimbo kuu la New York.
Mpango wa kufunga makanisa ni sehemu ya mchakato wa kubadili sura na mwelekeo wa kanisa la new York Kiutendaji ulioanza mwaka 2010.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times makanisa yatakayofungwa yatatamkwa kesho Jumapili.
 Tayari vuguvugu la upinzani dhidi ya hatua hiyo zimeanza hasa kw amakanisa ambayo yanaonesha yapo katika hatari kw akutofikia vigezo vilivyowekwa na watawala.
Jimbo kuu lina parokia 368 katika maeneo ya Bronx, Manhattan, kisiwa cha Staten  na kwenye kaunti saba  zilizopo kaskazini mwa Jiji.
 Mwaka 2007, kadinali Edward M. Egan alifunga parokia 21 na kuzua sokomoko kubwa miongoni mwa waumini ambalo bado linaendelea katika baadhi ya parokia hizo.
 “baadhi ya waumini wetu watahuzunika,watachanganyikiwa na hata kukasirika,” Mrithi wa kadinali Egan kama Askofu Mkuu,Kadinali Timothy M .Dolan aliandika katika gazeti la wakatoliki wa New York kuhusiana na mabadiliko hayo.
Alisema anaelewa kuhusu hali hiyo kwani wengi wa waumini wanatambua kwamba parokia hizo ndio mama wa imani.Alisema wakatoliki wanathamini paroki zao na hilo litawauma sana.
Imeelezwa kuwa sababu za kufunga parokia hizo ni zile zile za mwaka 2007 ikiwamo ya kupungua kwa idadi ya mapadri wa kuhudumia kartika parokia,tatizo la kifedha kupungua kwa idadi ya wakatokliki wanaobatizwa na kuoa au kuolewa kanisani.
Dayosisi ya Brooklyn  ambayo hujumuisha na Queens, ilikabiliwa na tatizo hilo hilo na kuchukua hatua za kufunga baadhi ya parokia zake  kufikia 187  kutoka 199  kwa mwaka 2009.
“hatuna fedha kila mwaka kutoa dola milioni 40 kusaidia parokia zisizohitajika,” alisema Kadinali Dolan katika blogu yake mwaka jana.
Kwa mujibu wa habari za ndani paroko wanaohusika na kufungwa kwa parokia zao wameambiwa hali hiyo Ijumaa iliyopita na leo katika makanisa yote kutakuwa na taarifa.
Mwaka mmoja uliopita, wakishauriwa na watu kutoka nje waliajiriwa na kanisa, walitembelea kila parokia ambapo waliomba ikusanye waumini wake kuangalia uwezo wao na udhaifu wao na kujadiliana na parokia jirani kuhusu walichiokiona katika majadiliano kuhusu parokia yao.
Baadaye kamati za ushauri ambazo zilijumuisha mapadri na waumini wa kawaida zilipitia taarifa hizo na kuzitolea mapendekezo Aprili mwaka huu.
Mapendekezo hayo yalifika kwa kadinali Juni mwaka huu.
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

Post a Comment

أحدث أقدم