
Vyama vya upinzani na mashirika yasio ya kiserikali ya Burkina Faso
yameitisha maandamano makubwa Jumapili ili kupinga uwamuzi wa jeshi
kuchukua uwongozi wa serikali ya mpito.
Mkuu wa majeshi Jenerali Nabere Honare Traore, alitangaza Jumamosi
kwamba, baraza la wakuu wa majeshi kwa sauti mmoja limemteuwa luteni
kanali Isac Yacouba Zida kuongoza serikali ya mpito kwa mwaka moja.
Katika taarifa aliyotowa ameeleza kwamba luteni kanali Zida atakutana
na viongozi wa upinzani na wa mashirika ya kiraia kwa mashauriano juu
ya kuunda serikali ya mpito.
Uwamuzi huo haujawaridhisha viongozi hao wa upinzani na wakiraia
kwani kufuatana na katiba ya Burkina Faso, pindi rais atakapoacha
madaraka rais wa bunge la taifa anabidi kuchukua nafasi yake kwa muda
hadi kuitishwa uchaguzi mwengine wa rais.
Hatua hiyo hitowezekana, kutokana na uwamuzi ulochukuliwa na wakuu wa
jeshi kulivunja bunge na kusitisha katiba ya nchi. Viongozi wa upinzani
wanashikilia kwamba ni lazima kwa serikali ya mpito kuongozwa na raia.
Wakati huo huo Rais Aliassane Outara wa Ivory Coast ametangaza kwamba
serikali yake imempokea rasmi Bw. Compaore, familia yake, na washauri
wake wa karibu.
Taarifa yake inaeleza kwamba taifa hilo jirani linawasi wasi kutokana
na hali inayoendelea huko Burkina Faso na kuwatakia wananchi wake
kuchukua hatua za busara zitakazo dumisha amani na utulivu.
إرسال تعليق