![Alama za mauaji yaliyotokea Mandera](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/304/amz/worldservice/live/assets/images/2014/11/23/141123182843_bbc_304x171_bbc_nocredit.jpg)
Makamo wa rais wa Kenya, William Ruto, anasema kuwa askari wa usalama
wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa al-Shabaab hadi kwenye kambi yao
nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi kaskazini-mashariki mwa
Kenya hapo jana ambapo raia 28 waliuliwa.
Bwana Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni mbili tofauti.Alisema kambi ya al-Shabaab iliangamizwa.
Habari hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Gavana wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuwalinda raia.
Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio.
- bbc
إرسال تعليق