KIVUKO KIPYA CHA MSANGAMKUU CHAWASILI MKOANI MTWARA
Hisia0
Kivuko
cha Msangamkuu( MV Mafanikio) chenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 50
pamoja na abiria 100 kikiwasili Mkoani Mtwara tayari kwa kuanza kazi
rasmi ya kutoa huduma kati ya upande wa Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Kivuko
kipya cha (MV Mafanikio) kama kinavyoonekana mara baada ya Serikali
kutekeleza ahadi yake ya kuwaletea wananchi wa Mtwara Kivuko hicho
kipya. Wananchi
wakikimbia kuingia ndani ya Kivuko hicho kipya cha (MV Mafanikio) huku
wakishangilia kuonyesha furaha yao mara baada ya kivuko hicho kuwasili
mkoani Mtwara. Baadhi ya kina mama nao walipata fursa ya kukaa na kufurahia ndani ya kivuko hicho kipya. Usafiri huu wa Mitumbwi ndio uliokuwa unategemewa na wananchi hao wa Mtwara kabla ya ujio wa Kivuko kipya cha Msangamkuu. Mkurugenzi
wa Ufundi na Umeme (DTES) Dkt. Wiliam Nshama kutoka Wizara ya Ujenzi
akipita kukagua Kivuko hicho kipya cha Mv Mafanikio. Picha zote kwa
Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
إرسال تعليق