Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa
ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika.
Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner.
Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu
aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa
ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa.
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote
amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye
huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti
au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya
nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu
wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema.
Ninavyofikiria mtu anayenipenda mimi alinijua sababu ya muziki na
waendelee kuliheshimu hilo, kwasababu kila mtu ana haki ya kuwa na
privacy. Ingekuwa kila mmoja angekuwa anatoka kwake anaanza kuelezea
mambo yake, mama yake jana walishinda njaa, au mume wake alimfanya hivi,
sidhani kama kuna mtu yeyote anapenda kuelezea maisha yake, hata
matatizo yake mbele za watu.”
“Kwahiyo mpenzi wako Gadner bado mko naye,” aliuliza mmoja wa
watangazaji wa kipindi hicho na mchekeshaji, MC Pilipili. “Swali
nafikiri hujalijibu, umemtosa, hujamtosa?,” aliuliza Fadhil Haule,
mtangazaji mwingine wa show hiyo.
“Nimemuacha,” alijibu Jide. “Huyu (Gadner) tumeshamalizana.”
Isikilize interview hiyo hapo chini.
Post a Comment