Mkapa kutunuku shahada 4,000 Chuo Kikuu Dom

Dodoma. Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa leo atawatunuku wahitimu 4,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) shahada mbalimbali.
Mkapa ataifanya kazi hiyo katika mahafali ya tano yatakayofanyika katika Viwanja vya Chimwaga mjini Dodoma.
Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, atawatunuku wanafunzi hao kwa awamu mbili, leo na kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake, Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliohitimu mwaka huu.
“Mbali na kuwatunuku wahitimu hao, Mheshimiwa Mkapa atapokea pia tuzo ya ushindi wa mwaka tuliyoipata kutoka vyuo vinavyofundisha lugha ya Kichina baada ya Udom kuibuka mshindi kati ya taasisi 400 ulimwenguni zinazofundisha lugha hiyo,” alisema Kikula.
Jana wasomi wa chuo hicho walikutana katika kongamano maalumu lililokuwa likijadili masuala mbalimbali, likiwamo suala la bima ya afya kwa wafanyakazi na mtoa mada katika kongamano hilo alikuwa Ailon Gesase
- Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post