VIJANA
watatu waliokuwa wanafanya kjazi ya kuchimba madini katika kiwanja kinachomilikiwa
na Mchimbaji mdogo aliyefahamika kwa jina la Christofer Simkoko wamekufa baada
ya kuangukiwa na kifusi cha udongo.
Taarifa
zilizotolewa na Msimamizi wa machimbo hayo yaliyopo katika eneo la Mto Muhuwesi
maarufu kwa jina la namba saba Bw. Hamisi Ibrahim Yasini alisema kuwa tukio
hilo lilitokea majira ya saa 4.30 asubuhi ya Novemba 20 mwaka huu .
Bw.
Yasini aliendelea kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea wakati vijana hao wakitoa
udongo wenye madini ya vito ( Veny).
Alisema
baada ya kutokea kwa tukio hilo yeye kwa kushirikiana na wachimbaji wengine
walijitahidi kujaribu kuokoa maisha ya wenzao kwa kuanza kuchimba na kutoa
udongo huo kwa kutumia chepe na mikono hali ambayo iliwafanya washindwe
kuwaokoa wakiwa wazima kutokana na kutokuwa na nyenzo zenye uwezo mkubwa
kiutendaji.
Kwa
mujibu wa Ibrahi wachimbaji waliopoteza maisha ni wakazi wa Wilaya ya Vijiji
vya Wilaya ya Tunduru na kuwataja kuwa ni Rashid Sandali (30) mkazi wa Kijiji
cha Legezamwendo,Ibrahim Husein (34) mkazi wa kijiji cha mwongozo na Kaluma
Ally (35) Mkazi wa kijiji cha Namasalau wilayani humo.
Akizungumza
na wachimbaji wa madini hayo alipotembelea katika eneo la tukio hilo Mwenyekiti
wa kamati ya Ulinzi na usalama na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Bakari
Nalicho pamoja na mambo mengine alisema Pamoja na Serikali kupenda watu wake
kupenda wapate fedha ili kuendesha maisha yao kwa kula raha na starehe, lakini
haiwezekani kuona wananchi wake wakipoteza maisha kama lilivyo tokea tukio hilo
kwa kisingizio cha kutafuta fedha.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Mihayok Msikhela pamoja na
kudhibitisha kuwepo kwa tukio hilo aliwataka wachimbaji katika mkoa wake
kuzingatia taratibu za uchimbaji wa madini hayo pamoja na kuzingatia maelekezo
na taratibu za uchimbaji salama.
Source:
Steven Chindiye, Tunduru
إرسال تعليق