HALI
tete, siku chache baada ya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam,
Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama Chonji kukamatwa na kutupwa
gerezani kwa tuhuma za kukamatwa na dawa kulevya, sasa mali zake
zimeanza kuchunguzwa.
Mfanyabiashara
maarufu jijini Dar es Salaam, Muharani Mohammed Abdallah, maarufu kama
Chonji(mwenye suti), akiwa chini ya ulinzi.
Vyanzo vyetu makini kutoka jeshi la polisi zinasema kuwa mali
zinazochunguzwa kutokana na tuhuma hizo nzito ni maghorofa, fedha pamoja
na magari anayomiliki. “Tuliambiwa kuwa huyu bwana alikuwa akiishi
maisha ya hali ya juu, sasa kutokana na tuhumza zake polisi wameanza
kuchunguza kila alichonacho ili kujua uhalali wake,” kilisema chanzo.Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo akiwemo mtoto wa meya mmoja wa zamani (jina tunalihifadhi), jijini Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa alikuwemo katika mkumbo wa kukamatwa Chonji lakini alitoroka na sasa anasakwa na polisi.
Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na
Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa alipotafutwa
na gazeti hili ili afafanue madai hayo alisema uchunguzi wa mali za wote
wanaotuhumiwa kukamtwa na dawa za kulevya ni lazima ufanyike.
Chonji akiwa chini ya ulinzi mkali na wenzake mahakamani.
“Tunachunguza mali zao wote waliokamatwa na tuhuma za dawa za kulevya
na siyo kwa Chonji peke yake, inapodhihirika kuwa ni za madawa huwa
wanafilisiwa,” alisema Kamanda Nzowa. Chonji na wenzake wanne
walikamatwa usiku wa manane Oktoba 21, mwaka huu nyumbani kwake Magomeni
Mtaa wa Kondoa jijini Dar na inadaiwa walikuwa na mzigo wa unga
uliokuwa ukifungwa katika vifurushi vidovidogo pia anadaiwa kukutwa na
sare za jeshi (JWTZ) na bastola.
إرسال تعليق