Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili hivi
karibuni, Nabo alisema alifunga ndoa na Mariana mwaka 2002 na kujaliwa
kupata watoto wawili, Madelin na Joyce Nabo na ndani ya miaka 13 ya
ndoa waliishi kwa amani.
“Visa vilianza hivi karibuni baada ya mimi
kupata hundi ya shilingi milioni 50 kupitia kazi zangu za ufundi wa
kusuka mashine za magari, za kusaga na kukoboa na za
matofari.“Nilimuonesha mke wangu hundi ili tupange tuzifanyie nini fedha
hizo, lakini baada ya siku mbili hundi ikiwa benki kusubiri iwe tayari
kutumika, nilianza kuumwa vitu visivyoeleweka na kuishiwa nguvu.
“Nilikimbizwa Hospitali ya Aga Khan (Dar) na kugundulika kuwa nilipewa sumu kwenye chakula.
“Nilimuuliza mke wangu ni nani atakuwa ameniwekea sumu akasema sijui. Siku nyingine nilimkuta ana dawa za ajabuajabu, nikamkalisha chini na kumsema aachane na habari za dawadawa.
“Nilishangaa sana kwani mambo mengi mke wangu alianza kuyafanya kuanzia hapo. Niligundua pia kwamba alikuwa akichukua nguo zake kidogokidogo na kuhamishia sehemu nyingine, ndipo siku moja akatoroka nyumbani moja kwa moja.

“Nilijaribu kumsihi mke wangu arudi kwa ajili ya watoto lakini kwake imekuwa ngumu. Nimeeleza haya ili jamii imfahamu ni mwanamke wa aina gani kwani hana huruma, maana nilishangaa hata alipoondoka watoto walifurahi,” alisema Nabo.
Mariana alipotafutwa ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo ya mumewe hakupatikana, waandishi wetu wanaendelea kumsaka.
إرسال تعليق