Kutengeneza uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye
changamoto kubwa. Japo hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na
rahisi ambayo unaweza kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka
desturi ya kusema mambo haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa
couple itakayowapa wivu marafiki zetu.
1. Nakupenda

Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako.
Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi
wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini
mko pamoja.
2.Nilikuwa nakuwaza

Ni muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko
sehemu moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako
ambacho kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?

Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za
kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi
kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu
zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa
pamoja.
4. Nakuunga mkono

Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake.
Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo
aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu
mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu,
kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha
uhusiano wenu.
5.Umependeza
Picha na OGS Studio
Picha na OGS Studio
Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau
katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia.
Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie
vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
6. Samahani

Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea
maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna
nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya
kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za
mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.
7. Hakuna kama wewe

Mpenzi wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye,
basi hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye
ni bora na hakuna kama yeye.
8. Napenda mawazo yako
Picha: OGS Studio
Mwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.
9.Nakuheshimu

Kama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na
mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo
yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na
salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10. Napingana na hilo


Sehemu moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale
usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila
kitu na hakuna mwanamke anayetaka kuzaa watoto na mwanaume asiye na
msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye
mawazo na matendo ya kila mmoja. Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo
wa heshima. Kumpa mpenzi wako mtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata
suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.
11. Usiku mwema

Tunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno. Kwa
kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka bahari, hivyo hakuna
kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’ mwema.
Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana, maliza siku na kishindo chanya.
Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana, maliza siku na kishindo chanya.
Chanzo: Lifehack
إرسال تعليق