
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumamosi, Novemba Mosi, 2014, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Meja
Jenerali Aidan Isidori Mfuse kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo, mjini Dar Es Salaam.
Meja
Jenerali Mfuse ambaye nambari yake ya usajili wa Jeshi ilikuwa P1624 alifariki
dunia Jumatano, Oktoba 29, 2014, katika Hospitali ya Apollo, nchini India,
ambako alikuwa anatibiwa.
Rais
Kikwete amewasili kwenye Hospitali ya Lugalo (GMH) kiasi cha saa tano asubuhi kujiunga
na waombolezaji wengine akiwamo Rais wa Tatu wa Tanzania, Mheshimiwa Benjmin
William Mkapa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mheshimiwa Dkt.
Hussein Mwinyi na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Meja
Jenerali Aidan Isidori Mfuse alizaliwa Julai Mosi, mwaka 1948, mkoani Njombe na
alipata uofisa wa Jeshi Desemba 23, mwaka 1972, alipopandishwa kuwa Luteni.
Alistaafu Jeshi Juni 30 mwaka 2007 baada ya kuwa amelitumikia miaka 34, miezi
minne na siku 13.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1
Novemba,2014

Post a Comment