MAREHEMU MEJA JENERALI AIDAN ISIDORE MFUSE AAGWA DAR LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Novemba Mosi, 2014, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Meja Jenerali Aidan Isidori Mfuse kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo, mjini Dar Es Salaam.
Meja Jenerali Mfuse ambaye nambari yake ya usajili wa Jeshi ilikuwa P1624 alifariki dunia Jumatano, Oktoba 29, 2014, katika Hospitali ya Apollo, nchini India, ambako alikuwa anatibiwa.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Mhe
Benjamin William Mkapa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt
Hussein Mwinyi, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni
Jenerali Samuel Ndombe wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali
Aidan Isidore Mfuse katika hospitali kuu ya JWTZ ya Lugalo jijini Dar
es slaam leo Novemba 1, 2014  kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda
Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumapili Novemba 2,
2014

Rais Kikwete amewasili kwenye Hospitali ya Lugalo (GMH) kiasi cha saa tano asubuhi kujiunga na waombolezaji wengine akiwamo Rais wa Tatu wa Tanzania, Mheshimiwa Benjmin William Mkapa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange.
Meja Jenerali Aidan Isidori Mfuse alizaliwa Julai Mosi, mwaka 1948, mkoani Njombe na alipata uofisa wa Jeshi Desemba 23, mwaka 1972, alipopandishwa kuwa Luteni. Alistaafu Jeshi Juni 30 mwaka 2007 baada ya kuwa amelitumikia miaka 34, miezi minne na siku 13.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Novemba,2014

Post a Comment

أحدث أقدم